![]() |
Kaimu Mkurugenzi wa Habari na Uhusiano Makao Makuu ya Jeshi (JWTZ),Luteni Kanali Gaudentius Gervas Ilonda akizungumza na waandishi wa habari Leo Agosti 24,2023 Jijini Dodoma. |
![]() |
Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa,akizungumza na waandishi wa habari Leo Agosti 24,2023 Jijini Dodoma. |
Na Okuly Julius-Dodoma
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limetoa siku Saba kwa wananchi, wafanyabiashara
Na Wasanii kuacha kutumia Mavazi ya kijeshi au yanayoelekea kufanana na sare za kijeshi.
Limesema baada ya siku Saba hatua Kali zitaanza kuchukuliwa hivyo Kwa mwenye aina yeyote ya Sare hizo huku likiwataka wazipeleke katika kambi yeyote iliyo karibu na maeneo yao kwakuwa hawatahojiwa walipozipata.
Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari Leo Agosti 24,2023 Jijini Dodoma Luteni Kanali Gaudentius Gervas Ilonda Kaimu Mkurugenzi wa Habari na Uhusiano Makao Makuu ya Jeshi (JWTZ) amesema matumizi ya sare za jeshi ni kinyume cha sheria na katazo hilo ni kwa mujibu wa lifungu cha 9998 cha sheria ya ulinzi wa Taifa (NDA) sura 192 sheria namba 24 ya mwaka 1966 iliyofanyiwa marejeo mwaka 2092. Aidha kifungu cha 178 cha sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16 ( Penal Code) na kifungu cha 6 cha sheriia ya Usalama wa Taifa , vinakataza raia kuvaa sare na mavazi ya majeshi ya ulinzi au yanayofanana nayo.
“Zipo baadhi ya Taasisi zinazowashonea watumishi wake sare na aina hiyo, wapo pia wafanyabiashara wanaoingiza nchini mavazi ya aina hiyo na kuyauza kwa baadhi ya raia kupitia katika maduka au maeneo yao ta buashara , aidha wapo baadhi ya wasanii wanaovaa mavazi hayo na kuyatumia wawao kwenye majukaaa ya kazi zao bila kufuata utaratibu,” ameongeza kaa kusema.
Luteni Kanali Ilonda ameendelea kwa kusema Kumekuwa na wimbi kubwa la baadhi ya wananchi wanaokamatwa au kuonekana wakiwa wamevaa sare za jeshi la ulinzi la wananchi wa Tanzania au mavazi yanayofanana na sare za kijeshi .
“ Wapo baadhi ambao kwa kuyatumia mavazi hayo wamekuwa wakiwawatapeli wananchi na wengine kufanya vitendo viovu ambao pia wamekuwa wakidhaniwa kuwa ji wanajeshi, Vitendo hivyo ni uvunjifu wa sheria za nchi, hivyo havipaswhli kufumbiwa macho , aidha hali hii ikiachwa kuendelea inaweza kuhatarisha ulinzi na usalama wa nchi yetu ,” amesema Luteni Kanali Ilonda.
Pia amesema mahusiano ya jeshi na wananchi ndio mhimili mkubwa ndani na nje ya nchi hivyo si hekima kulumbana kwa namna yoyote ile na baadhi ya wananchi wenye mavazi yaliyokatazwa .
“Ndio maana tunatoa siku saba kuyasalimisha bila kuchukuliwa hatua ili kuepuka usumbufu, kwa ambaye hatawasilisha atakuwa na nia ovu na dhamira mbaya,”.
Kwa upande wake Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa ametoa wito kwa wananchi kuhakikisha wanazingatia agizo hilo na wazazi wakague mabegi ya watoto wao ili kubaini kama kuna nguo ama vitu vinavyoendana na jeshi hilo ili wavisalimishe.
No comments:
Post a Comment