KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA AFYA YA MASUALA YA UKIMWI YAIPONGEZA OFISI YA WAZIRI MKUU - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, October 12, 2023

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA AFYA YA MASUALA YA UKIMWI YAIPONGEZA OFISI YA WAZIRI MKUU

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Afya na Masuala ya UKIMWI Mhe Stansilaus Nyongo akizungumza na vijana wanaotekeleza Miradi ya Dreams na kuwapongeza kwa kazi nzuri wanayoifanya na kuwataka wasirudi nyuma ili wasijepoteza malengo yao ikiwa ni pamoja na kuendelea kuwashawishi wenzao ambao bado hawajapata elimu hiyo ili kuwaepusha na Maambukizi ya VVU.
Naibu waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Mhe Ummy Nderiananga akifurahia vyungu vinavyotengezwa na vijana wa kikundi cha Juhudi kupitia mradi wa Dreams Mkoani Shinyanga wakati wa ziara ya kamati yaKudumu ya Bunge ya Afya na Masuala ya UKIMWI ilipotembelea Miradi hiyo tarehe 11 Octoba,2023.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe Christina Mdeme akifurahia kazi za vijana wa Dreams wanazotengeneza Mkoani mwake na kuahidi kuwashirikisha kwenye Mkutano wa Jukwaa la akina mama linalotarajiwa kufanyika Mkoani humo kwa lengo la kupata uzoefu kwa upande wa masoko,Mkuu wa Mkoa aliambatana na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na Masuala ya UKIMWI walipokuwa wakikagua shughuli za UKIMWI zinazotekezwa Mkaoani Shinyanga, tarehe 11 Octoba,2023.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na Masuala ya UKIMWI Mhe Stanslaus Nyongo akiwa katika Picha ya Pamoja na Baadhi ya wawakilishi wa Mashirika yasiyo ya kiserikali yanayotekeleza programu ya Dreams Mkoa wa Shinyanga aliyekaa Kulia kwake ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe Ummy Nderiananga na Kushoto kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Chritina Mdeme,tarehe 11 Octoba,2023
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge na Uratibu Mhe Ummy Nderiananga akizungumza na vijana (hawapo katika picha) kutorudi nyuma kwani serikali haipo tayari kuona vijana wa Nchi hii wanajihusisha na masuala ya kuwaingiza katika mmomonyoko wa maadili na ndio maana Miradi ya kujikimu kiuchumi imeanzishwa,ili kila mmoja aweze kuwa na kitu cha kumwingizia kipato,aliyekaa kulia kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Afya na masuala ya UKIMWI Mhe Stanslaus Nyongo na kulia kwake ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TACAIDS Dkt.Jerome Kamwela.
Vijana wa Dreams wakionesha namna wanavyotengeneza vyungu na Majiko kwa kutumia Udongo wakati wa Ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge na Masuala ya UKIMWI walipotembelea MKoa wa Shinyanga kuona shuhghuli za UKIMWI zinavyotekelezwa .
Vijana kutoka kikundi cha Jahazi kinachowezeshwa na Programu ya Dream wakielezea namna wanavyotengeneza sabuni walipotembelewa na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na Masuala ya UKIMWI anayefuatilia ni Mhe .Dkt Christina Mzava,Mkoani Shinyanga tarehe 11 Octoba,2023.

Na Mwandishi wetu - Shinyanga

Kamati ya kudumu ya Bunge ya Afya na Masuala ya UKIMWI imeipongeza Ofisi ya Waziri Mkuu kupitia Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) kwa mafanikio makubwa katika kutekeleza afua za VVU na UKIMWI nchini.

Pongezi hizo zimetolewa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Stanslaus Nyongo wakati kamati ilipofanya ziara ya kutembelea na kukagua Mpango wa Dreams kupitia Mradi wa Epidemic Control (EPIC) unaotekelezwa na Shirika la Family Health International (FHI360) kwa wasichana balehe na wanawake vijana (AGYW) katika katika Mkoa wa Shinyanga.

Akizungumza mara baada ya kukagua vikundi vya vijana vikiwemo Sitetereki kilichopo Kata ya Old Shinyanga, Jahazi, Kata ya Ibadakuli na Tunaweza katika Kata ya Kolandoto Mhe. Nyongo amesema lengo la ziara ni kujionea maendeleo ya mradi huo na kuishauri Serikali maeneo ya kuboresha ili kuendeleza jitihada za kuwa na vijana wenye afya nzuri wanaoshiriki katika shughuli za uzalishaji na kujiletea maendeleo yao.

“Tunapongeza kazi kubwa inayofanywa na Rais wetu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kutoa maelekezo ya kumlinda mtoto wa kike hasa katika gonjwa kubwa la UKIMWI, namna ya kumkomboa mtoto wa kike, kujifunza kazi za ujasiliamali ili kujikwamua katika maisha pamoja kupaza sauti dhidi ya unyanyasaji wa kijinsia hivyo sisi kama wabunge tumeridhishwa na kazi inayofanywa na Serikali,”Amesema Mwenyekiti huyo.

Pia ametumia nafasi hiyo kumpongeza Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi. Christina Mndeme kwa kushirikiana na watendaji wake kuhakikisha wanatekeleza Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kufikia lengo la Serikali la kuwainua vijana ambao wamekuwa nguvu kazi kubwa ya maendeleo ya Taifa.

Aidha Mhe. Nyongo ameihimiza Halmashauri kuendelea kutoa mikopo ya Asilimia 10 ambapo asilimia nne hutolewa kwa vijana, wakati wanawake nao wakipatiwa asilimia nne na asilimia mbili kwa watu wenye ulemavu hatua itakayowawezesha kuboresha mitaji yao na kuongeza mnyororo wa thamani ya bidhaa zao.

“Kamati imefurahishwa na mafanikio katika afua zote ikiwemo upimaji wa VVU, Utoaji wa ARV, Uelimishaji, manunuzi na usambazaji wa vitendanishi na matumizi ya kinga pamoja na uwezeshaji kiuchumi kwa vijana hawa kupitia vikundi vyao,”Ameeleza.

Naye Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Mhe. Ummy Nderiananga amewaomba vijana wa kike kuendelea kujiamini , kufanya kazi vizuri kwani Serikali ya Awamu ya Sita inawajali vijana na kutambua mchango wao mkubwa katika Maendeo ya Taifa.

Akizungumzia ziara hiyo Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na Masuala ya UKIMWI Mhe. Hassan Mtenga ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa fedha za kukamilisha na kujengwa kwa miradi mikubwa ya maendeleo huku akiipongeza TACAIDS na wadau wa maendeleo kuwa na mwamko wa kuwawezesha vijana kujikwamua kiuchumi.

“Tumejifunza kitu kwasababu tunao watu wako tayari kupiga vita janga kuu la UKIMWI na niishukuru TACAIDS, Mawaziri wenye dhamana na hawa wadada ambao wameamua kutoka kwenye sughuli za kuuza bar na kuanzisha biashara zao sasa uwe mfano wa kuigwa kwa maeneo mengine,”Amepongeza Mhe. Mtenga.

Vilevile Mjumbe wa Kamati hiyo Mhe. Christina Mnzava amesema wazazi na walezi wana wajibu wa kusimamia malezi sahihi ya watoto ili kuwakomboa katika tabia hatarishi huku akiupongeza Mpango wa Dream kwa kuamua kuwafikia mabinti katika maeneo yao akishauri mradi huo kuongeza wigo na kuwafikia vijana wengine waliopo Vijijini .

“Sisi kama wazazi na walezi tunaweza kuwakomboa watoto wetu katika tabia hatarishi ambazo wanazipata mtaani kuna wengine walikuwa wanauza miili yao, lakini kutokana na mradi huu wamejikwamua wamefundishwa ujasiriamali, kuwekeza tumeona wasichana wamejitambua wanatengeneza sabuni, batiki, vyungu katika vikundi vya Kata za Old Shinyanga, Ibadakuli na Kolandoto kwa kweli wamefanya vizuri,”Ameeleza Mjumbe huyo.

Kwa upande wake Mshauri Mwandamizi wa Mpango wa Dreams kupitia Mradi wa Epidemic Control (EPIC) unaotekelezwa na Shirika la Family Health International (FHI360) Bi. Agnes Junga amefafanua kuwa lengo la Mpango huo ni kupunguza maambukizi ya Virusi vya UKIMWI kwa wasichana kuanzia umri wa miaka Tisa hadi 24.

“Mpango huu ulizinduliwa 2014 ukilenga kupunguza maambukizi ya virusi vya UKIMWI kwa Nchi 13 za Bara la Afrika ikiwemo Tanzania ambapo tulianza na Halmashauri Sita na hadi sasa tumefikia Halmashauri 12.

Shirika la (FHI360) kwenye mradi wa EPIC tunatekeleza Dreams katika Mikoa miwili ya Shinyanga ndani ya Halmashauri Tano na Iringa katika Halmashauri mbili na tunawafikia wasichana kuanzia miaka 15 hadi 25 walio nje ya shule pamoja na wazazi au walezi na jamii kwa ujumla tuhakikishe msichana anafikia ndoto zake.

Aidha akizungumza kwa niaba ya wanakikundi kutoka Vikundi vya Mabinti Balehe na Wanawake Vijana vya Sitetereki, Tunaweza na Jahazi mwanakikundi Sungi Leonard amesema uanzishwaji wa vikundi hivyo vimewasaidia kama mabinti kujitambua, kufahamu elimu ya afya, kuwajengea uwezo wa kukabiliana na vitendo vya kikatili pamoja na kuchukua tahadhari dhidi ya maambukizi mapya ya VVU na kuwawezesha kiuchumi .

“Nilikutana na mwezeshaji kiuchumi na mwelimishaji rika nikapata elimu ya ukatili wa kijinsia, umuhimu wa upimaji wa afya, matumizi sahihi ya kinga, magonjwa ya ngono na VVU ambayo imenisaidia kujitambua kama binti. Pia nilifanikiwa kujiunga katika kikundi cha Sitetereki nikajifunza kutengeneza batiki kazi ambayo inanipatia kipato na ninamudu mahitaji yangu tofauti na ilivyokuwa awali,”Ameshukuru Mwanakikundi huyo.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe Chritina Mndeme amesema Serikali ipo tayari kushirikiana na Mashirika yasiyokuwa ya kiserikali kuondoa katika kutoa elimu ya unyanyapaa na ubaguzi kwa watu wanaoishi na VVU ambao upo juu,kuwajengea vijana uwezo wa kiuchumi ili muda mwingi wautumie kwenye uzalishaji na sio kwenye mambo yanayoweza kuwasababishai maambukizi ya VVU,kuelimisha jamii kuacha mila potofu ambazo zinasababisha ukatili wa kijinsia.

No comments:

Post a Comment