NAIBU KATIBU MKUU NISHATI AWASILI OFISINI RASMI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Monday, March 11, 2024

NAIBU KATIBU MKUU NISHATI AWASILI OFISINI RASMI


Na Mwandishi Wetu Dodoma

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Dkt. James Mataragio amewasili rasmi ofisini na kuahidi kumsaidia Rais, Mhe. Samia Suluhu Hassan kutimiza malengo yake kwa Taifa.

Alipowasili Ofisi za Wizara eneo la Mtumba jijini Dodoma, alipokelewa na Katibu Mkuu Wizara hiyo Mha. Felchesmi Mramba, menejimenti na watumishi wengine wa Wizara ya Nishati.

Akizungumza mara baada ya mapokezi, Dkt. Mataragio amesema ushirikiano miongoni mwa wafanyakazi ni nyenzo muhimu ya kuyafikia matarajio ya viongozi wa kitaifa na Taifa kwa ujumla.

"Mimi nashukuru kuteuliwa kutumikia nafasi hii, nitaendelea kushirikiana na watumishi wenzangu ili kumsaidia Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kutimiza malengo yake." Amesema Dkt. Mataragio.


No comments:

Post a Comment