Miili ya watu wawili imeopolewa kutoka kwenye lori nyekundu, iliyokuwa imezama chini ya maji ambapo daraja la Baltimore liliporomoka.
Wafanyakazi wanane wa ujenzi walikuwa kwenye daraja hilo wakati meli ilipoigonga, na kuwatumbukiza kwenye majini.
Wawili kati ya wafanyikazi waliokolewa siku hiyo, lakini shughuli ya utafutaji inaendelea kwa wengine wanne - wote wakidhaniwa wamefariki.
Wafanyakazi wa uokoaji wanafanya kazi kushughulikia nyenzo hatari na wachunguzi wa ajali wako kwenye eneo la tukio.
Wanne kati ya waathirika sita wa kuporomoka kwa daraja hilo wametambulika kufikia sasa.
Katika mkutano na waandishi wa habari Jumatano, Polisi wa Jimbo la Maryland walimtambua Alejandro Hernandez Fuentes, 35, na Dorlian Ronial Castillo Cabrera, 26, kama wafanyikazi hao wawili waliopatikana na wapiga mbizi kutoka ndani ya lori.
Bw Fuentes anatoka Mexico na Bw Cabrera anatoka Guatemala.
Lakini wapiga mbizi hawawezi tena kuabiri maji kwa usalama kwa sababu ya saruji na uchafu uliopatikana mtoni, polisi walisema. Sasa wanatumia skana za sonar na wanaamini kuwa magari ambayo yanaweza kuwa na miili mingine "yamefunikwa kwa muundo wa juu na simiti" ambayo ilishuka kutoka kwenye daraja, afisa mmoja alisema.
Waathirika wengine wawili waliotoweka, ambao wanadhaniwa kufariki, pia wametajwa: Miguel Luna, mwenye asili ya El Salvador, na Maynor Suazo Sandoval, raia wa Honduras.
Wizara ya Mambo ya Nje ya Mexico ilisema awali kwamba raia wake wawili walidhaniwa kuwa wamefariki - mmoja wao ambaye sasa anajulikana kama Bw Fuentes - huku mwingine akiokolewa kutoka kwa maji.
Mtu mmoja ambaye alikuwa hospitalini baada ya kuopolewa ndani ya maji aliruhusiwa Kwenda nyumbani, maafisa walisema Jumatano jioni.
No comments:
Post a Comment