WAZIRI MKUU WA HAITI ARIPOTIWA KUJIUZULU. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Tuesday, March 12, 2024

WAZIRI MKUU WA HAITI ARIPOTIWA KUJIUZULU.



Waziri Mkuu wa Haiti Ariel Henry amejiuzulu, mwenyekiti wa kundi la nchi za Caribbean amesema, kufuatia wiki za shinikizo zinazoongezeka na kuongezeka kwa ghasia nchini humo.


Inakuja baada ya viongozi wa kanda kukutana nchini Jamaica siku ya Jumatatu kujadili mpito wa kisiasa nchini Haiti.


Kwa sasa Bw Henry yuko Puerto Rico baada ya kuzuiwa na magenge yenye silaha kurudi nyumbani.

Alikuwa ameiongoza nchi hiyo tangu kuuawa kwa rais Julai 2021.


Akizungumza kufuatia mkutano huo mjini Kingston, mwenyekiti wa Jumuiya ya Caribbean na Rais wa Guyana Irfaan Ali alisema: "Tunatambua kujiuzulu kwake baada ya kuanzishwa kwa baraza la mpito la rais na kumtaja waziri mkuu wa muda."


Magenge yenye silaha kali yamedhibiti mitaa ya mji mkuu wa Haiti wa Port-au-Prince katika siku za hivi karibuni, yakitaka waziri mkuu huyo ambaye hajachaguliwa ajiuzulu.


Bw Henry alikuwa nchini Kenya kutia saini mkataba wa kutumwa kwa kikosi cha usalama cha kimataifa kusaidia kukabiliana na ghasia wakati muungano wa magenge uliposhambulia vituo vya polisi na kuvamia magereza mawili makubwa zaidi nchini Haiti.


Ndege iliyokuwa imembeba Bw Henry ilizuiwa kutua kufuatia msururu wa mashambulizi katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Haiti.


Ameelezea nia ya kurejea Haiti lakini hali ya usalama inahitaji kuimarishwa kabla hajaweza kufanya hivyo, kulingana na Marekani iliyokuwa kwenye mazungumzo mjini Kingston siku ya Jumatatu.


Afisa mkuu wa Marekani alisema Bw Henry alifikia uamuzi wa kujiuzulu Ijumaa wiki iliyopita lakini alikuwa akisubiri tangazo rasmi ili mazungumzo yafanyike.


Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Blinken alitoa $100m zaidi (254,240.74TZS) kwa kikosi cha usalama kinachoungwa mkono na Umoja wa Mataifa chenye askari 1,000 ambacho Kenya inatarajiwa kuongoza nchini Haiti.


Mchango uliopendekezwa wa Marekani kwa kikosi cha usalama sasa unafikia $300m (762,722.21TZS) kufuatia tangazo la Bw Blinken, na $33m (83,899.44TZS) zaidi zimetengwa kwa ajili ya misaada ya kibinadamu.


Kundi la Caricom la viongozi wa Caribbean, pamoja na Marekani na wawakilishi kutoka Haiti, pia walijadili mfumo wa mpito wa kisiasa.


Rais Ali alisema baraza la mpito la rais litakuwa na waangalizi wawili na wajumbe saba wanaopiga kura, wakiwemo wawakilishi kutoka miungano kadhaa, sekta ya kibinafsi na mashirika ya kiraia, na kiongozi mmoja wa kidini.


Baraza limepewa mamlaka ya "haraka" kumteua waziri mkuu wa muda, alisema, akiongeza kuwa yeyote anayenuia kugombea katika uchaguzi ujao wa Haiti hataweza kushiriki.


Baraza hilo linatarajiwa kuongoza Haiti kuelekea kwa uchaguzi wa kwanza tangu 2016. Bw Henry, aliyekuwa mamlakani tangu kuuawa kwa Rais Jovenel Moïse, alikuwa ameahirisha uchaguzi mara kadhaa, akisema usalama lazima urejeshwe kwanza.

No comments:

Post a Comment