Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya amewatoa hofu Waheshimiwa Wabunge kuhusu mpango wa Serikali wa utekelezaji wa miradi saba ya ujenzi wa barabara kwa utaratibu wa uhandisi, ununuzi, ujenzi na fedha (EPC+F) kuwa itatekelezwa kama ilivyopangwa.
Mhandisi Kasekenya amesema hayo Bungeni leo Aprili 17, 2024 wakati akijibu swali la Mbunge Viti Maalum, Mhe. Agnes Elias Hokororo aliyehoji kuhusu ujenzi wa barabara ya Masasi – Nachingwea – Liwale (km 175) kwa kiwango cha lami hasa baada ya kusainiwa mkataba wa EPC + F.
Kasekenya ameeleza kuwa Serikali ina dhamira ya dhati ya kuzijenga barabara zote zilizopangwa kutekelezwa kwa utaratibu wa EPC+ F kuanzia mwaka huu wa fedha 2023/24 na tayari Wakandarasi wapo katika maeneo ya mradi kwa ajili ya kazi za awali.
“Niwahakikishie wabunge pamoja na wananchi kuwa dhamira ipo na hizo barabara zote zitaenda kujengwa kwa kiwango cha lami kama ilivyopangwa”, amesisitiza Kasekenya.
Kuhusu ujenzi wa barabara hiyo, Kasekenya amesema kuwa kwa sasa Mkandarasi ameanza na anaendelea na usanifu wa kina huku taratibu za kupata fedha kwa ajili ya malipo ya awali zikiendelea.
Kasekenya amefafanua kuwa ujenzi wa miradi saba ya barabara kwa utaratibu wa EPC + F unahusisha kufanya usanifu wa barabara kabla ya kuanza ujenzi.
Ikumbukwe kuwa barabara ambazo zitajengwa kwa utaratibu huu wa EPC + F ni pamoja ba Barabara ya Kidatu – Ifakara – Lupiro – Malinyi – Kilosa Kwa Mpepo – Londo – Lumecha/Songea (km 435.8); Barabara ya Arusha – Kibaya – Kongwa (km 453.42); Barabara ya Handeni – Kiberashi – Kijungu – Kibaya – Njoro – Olboroti - Mrijo Chini – Dalai – Bicha – Chambolo – Chemba – Kwa Mtoro – Singida (km 384.33); Barabara ya Igawa – Songwe – Tunduma (njia nne) (km 237.9).
Nyingine ni Barabara ya Masasi – Nachingwea – Liwale (km 175); Barabara ya Karatu – Mbulu – Haydom – Sibiti River – Lalago – Maswa (km 339) ; na Barabara ya Mafinga – Mtwango – Mgololo (km 81).
Barabara hizo zitapita katika mikoa 13 ambayo ni Morogoro, Ruvuma, Arusha, Manyara, Dodoma, Tanga, Singida, Mbeya, Songwe, Lindi, Mtwara, Simi
No comments:
Post a Comment