OR - TAMISEMI
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) anayeshughulikia Elimu Mhe. Zainabu Katimba ameahidi kuendeleza ushirikiano na watendaji wa Ofisi ya Rais-TAMISEMI ili kutimiza azma ya Mhe. Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan ya kutoa huduma bora kwa wananchi.
Mhe. Katimba ametoa ahadi hiyo leo Aprili 5, 2024 Jijini Dodoma mara baada ya kuwasili Makao Makuu ya Ofisi ya Rais-TAMISEMI yaliyopo katika Mji wa Serikali Mtumba.
Mhe. Katimba ameahidi kuendelea kushirikiana kiutendaji na watumishi wote ili kutekeleza majukumu ya Ofisi ya Rais-TAMISEMI kwa uadilifu na weledi.
“Ninawaomba tushirikiane, nami ninaahidi kuwapa ushirikiano katika kutekeleza majukumu ya ofisi kwa lengo la kutoa huduma bora kwa wananchi” amesisitiza Mhe. Katimba
Naye, Naibu Waziri Ofisi ya RAIS –TAMISEMI anayeshughulikia Afya Dkt. Festo Dugange amewataka watumishi wa Ofisi ya Rais TAMISEMI kuhakikisha wanatoa ushirikiano kwa Mhe. Katimba ili aweze kutekeleza majukumu yake ipasavyo.
Mhe. Zainabu Katimba aliapishwa tarehe 04 Aprili 2024 Ikulu jijini Dar es Salaam na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa Naibu Waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI.
No comments:
Post a Comment