WADAU WA ELIMU WATAKIWA KUSHIRIKI KIKAMILIFU KATIKA KUPANGA MIPANGO YA MAENDELEO SEKTA YA ELIMU - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, April 3, 2024

WADAU WA ELIMU WATAKIWA KUSHIRIKI KIKAMILIFU KATIKA KUPANGA MIPANGO YA MAENDELEO SEKTA YA ELIMU

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Elimu ,Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo,akizungumza leo Aprili 3,2024 jijini Dodoma wakati akifungua Mkutano wa mwaka wa pamoja wa tathimini wa sekta ya elimu kwa mwaka 2023/24 wenye kaulimbiu kuwa Mageuzi katika Elimu kwa Maendeleo Endelevu kwa niaba ya Waziri wa Elimu ,Sayansi na Teknolojia Prof.Adolf Mkenda

NAIBU Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. James Mdoe,akielezea lengo la Mkutano wakati wa Mkutano wa mwaka wa pamoja wa tathimini wa sekta ya elimu kwa mwaka 2023/24 wenye kaulimbiu kuwa Mageuzi katika Elimu kwa Maendeleo Endelevu unaofanyika jijini Dodoma.

NAIBU Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Dk Charles Msonde,akizungumza wakati wa Mkutano wa mwaka wa pamoja wa tathimini wa sekta ya elimu kwa mwaka 2023/24 wenye kaulimbiu kuwa Mageuzi katika Elimu kwa Maendeleo Endelevu unaofanyika jijini Dodoma.

MKUU wa Kitengo cha Elimu Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) Dkt. Daniel Baheta ,akizungumza wakati wa Mkutano wa mwaka wa pamoja wa tathimini wa sekta ya elimu kwa mwaka 2023/24 wenye kaulimbiu kuwa Mageuzi katika Elimu kwa Maendeleo Endelevu unaofanyika jijini Dodoma.

MKURUGENZI wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TenMeT) Bi.Faraja Nyalandu ,akizungumza wakati wa Mkutano wa mwaka wa pamoja wa tathimini wa sekta ya elimu kwa mwaka 2023/24 wenye kaulimbiu kuwa Mageuzi katika Elimu kwa Maendeleo Endelevu unaofanyika jijini Dodoma.

SEHEMU ya Washiriki wakimsikiza Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu ,Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo (hayupo pichani) ,akizungumza wakati akifungua Mkutano wa mwaka wa pamoja wa tathimini wa sekta ya elimu kwa mwaka 2023/24 wenye kaulimbiu kuwa Mageuzi katika Elimu kwa Maendeleo Endelevu kwa niaba ya Waziri wa Elimu ,Sayansi na Teknolojia Prof.Adolf Mkenda


Na Okuly Julius-Dodoma 


WAZIRI wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Prof.Adolf Mkenda ametoa wito kwa Wadau wa Elimu kushiriki kikamilifu katika kupanga Mipango ya Maendeleo ya Elimu na program mbalimbali kwa lengo la kuhakikisha elimu inaleta maendeleo kwa mtu mmoja mmoja, jamii na Taifa kwa ujumla.


Hayo yamesemwa leo Aprili 3,2024 jijini Dodoma na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo,Prof. Carolyne Nombo,wakati akifungua Mkutano wa mwaka wa pamoja wa tathimini wa sekta ya elimu kwa mwaka 2023/24 wenye kaulimbiu kuwa Mageuzi katika Elimu kwa Maendeleo Endelevu kwa niaba ya Waziri wa Elimu ,Sayansi na Teknolojia Prof.Adolf Mkenda


Prof.Nombo amesema kuwa Mkutano huu utawawezesha Wadau kujadili changamoto mbalimbali, kuweka mikakati ya namna ya kukabiliana nazo, kuweka maazimio na mikakati mbalimbali ya Uboreshaji wa Elimu nchini.


"Nimatumaini yangu wadau wote mnaoshiriki katika Mkutano wa mwaka huu wa Tathmini ya Pamoja ya Maendeleo ya Sekta ya Elimu, mtatumia fursa hii kujadili kwa kina mawasilisho yatakayofanyika na kutoa maoni yenye tija katika kuboresha elimu yetu nchini."amesema Prof.Nombo


Amesema Kaulimbiu hiyo inaakisi mwelekeo wa Serikali katika mageuzi makubwa yaliyofanyika pamoja na yanayoendelea kufanyika ili Elimu iwe chombo cha Kimkakati katika kuleta Maendeleo Endelevu na kuwawezsha Watanzania kwendana na kasi ya mendeleo katika ulimwengu wa utandawazi .


"Wizara imefanya mageuzi makubwa kupitia: Mapitio ya Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014 na sasa tuna Sera ya Elimu na Mafunzo 2014, Toleo la 2023; na pia Mitaala Mipya ya Elimu ya Awali, Msingi, Sekondari na Ualimu."


Nakuongeza kuwa" Sera ya Elimu na Mitaala ndiyo nyenzo mama katika utoaji Elimu nchini, na hiwahakikishie uwa zimefanyiwa kazi kwa weledi mkubwa kwa kuzingatia mazingira yetu na hitaji la soko na zitawasilishwa kwa kina katika Mkutano huu. "


Aidha amesema kuendeleza Rasilimaliwatu ni moja kati ya majukumu ya msingi yanayotekelezwa na Wizara ya Elimu kwa kushirikiana OR – TAMISEMI na Wadau wa Sekta ya Elimu.


"Eneo hili linajumuisha kuandaa na kutekeleza programu na mikakati mbalimbali inayolenga kuendeleza maarifa na ujuzi wa rasilimaliwatu nchini, kuanzia ngazi ya elimu ya awali hadi elimu ya juu ili kuwawezesha vijana kujiajiri na kuajirika ndani na nje ya mipaka ya nchi yetu."amesisitiza


Hata hivyo ametoa rai kwa washiriki, kila mmoja kwa nafasi yake kushiriki kikamilifu katika tathimini hiyo ya pamoja ili Maazimio yatakayofikiwa na Mkutano huo yakawe Msingi thabiti wa utekelezaji wa ajenda ya Maendeleo Endelevu katika Sekta yetu ya Maendeleo.


Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Dk Charles Msonde amesema Serikali imefanya uwekezaji mkubwa katika sekta ya elimu na kuwa mkutano huo utakuwa ni fursa ya kuangalia hayo na kubainisha changamoto ili kuendelea kuboresha sekta hiyo ambayo ni muhimu katika mendeleo ya nchi.


Awali, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. James Mdoe amesema wadau kwa pamoja watajadili changamoto na mafanikio katika sekta ya elimu na hatimaye kuja na mikakati ya kuboresha sekta ya elimu.

No comments:

Post a Comment