WANAFUNZI WAMPONGEZA MATHAYO KWA KUWALETEA MADAWATI NA MEZA. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, May 23, 2024

WANAFUNZI WAMPONGEZA MATHAYO KWA KUWALETEA MADAWATI NA MEZA.


Na Ashrack Miraji, Same.

Leo Alhamisi Mei 23,2024, Diwani wa Kata ya Njoro, Omar Abeid, alikabidhi madawati na meza kwa uongozi wa shule ya sekondari Mighara. 


Lengo ni kuhakikisha wanafunzi wanapata mazingira bora ya kusoma salama na rafiki wakati wote wanapokuwa shuleni.


Mhe. diwani aliwasihi walimu na wanafunzi kuhakikisha wanatunza vifaa hivyo ili viweze kutumika vizuri.


Fedha za kununua madawati na meza hizi zilitoka kwenye mfuko wa Jimbo la Same Magharibi, ambazo Mhe. David Mathayo (Mb) aliwasilisha kwa wanafunzi.


Pamoja na hayo, aliwataka wanafunzi kuwaombea viongozi wa taifa, hasa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan na Mhe. David Mathayo (Mb), ili waweze kutimiza ndoto za elimu.


Mhe. diwani alisisitiza umuhimu wa kushukuru viongozi hao kwa kazi nzuri wanazofanya kuhakikisha wananchi wa jimbo la Same Magharibi wanapata huduma stahiki.


Khadija Said, mmoja wa wanafunzi wa shule hiyo, alitoa pongezi kwa Mhe. David Mathayo kwa kuboresha mazingira ya kusoma. 


Kabla ya hapo shule ilikuwa inakabiliwa na changamoto ya kukosa viti na meza na sasa wanafunzi wanaweza kusoma kwa utulivu na wanamuombea Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kujenga madarasa zaidi nchini kote kwani ni ishara ya uzalendo.






No comments:

Post a Comment