WAZIRI MHAGAMA ATETA NA WANAPERAMIHO - OKULY BLOG

Breaking

Home Top Ad

TANGAZA NASI HAPA | PIGA 0785 364 965

Sunday, May 5, 2024

WAZIRI MHAGAMA ATETA NA WANAPERAMIHO

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera Bunge na Uratibu ) Mhe. Jenista Mhagama (Mb) Peramiho akizungumza na wananchi wa Peramiho A katika Halmashauri ya wilaya ya Songea Mkoani Ruvuma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera Bunge na Uratibu ) Mhe. Jenista Mhagama (Mb) Peramiho akikabidhi mabati kwa uongozi wa soko la peramiho A ili ziweze kuezeka soko hilo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera Bunge na Uratibu ) Mhe. Jenista Mhagama (Mb)Peramiho akisalimiana na Godfey Mukanula Mwanachama mpya wa CCM kutoka Chama cha Demokrasia na maendeleo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera Bunge na Uratibu ) Mhe. Jenista Mhagama (Mb)Peramiho akilakiwa na wananchi wa Peramiho alipopita kusalimia.

Na Mwandishi wetu

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera Bunge na Uratibu ) Mhe. Jenista Mhagama (Mb) Peramiho amesema serikali kupitia Ofisi ya Rais TAMISEMI imetenga kiasi cha milioni 500 kwa mwaka ujao wa fedha kwa ajili ya Ujenzi wa kituko cha afya katika Kijiji cha Nguvu moja.

Amesema hayo Wakati alipopita kuwasalimia wananchi katika Kijiji cha Peramiho A kilichopo Halmashauri ya wilaya ya Songea Mkoani Ruvuma Leo tarehe 04/05/2024.

Ameongeza kusema Chama cha Mapinduzi ndicho Chama kinachohangaika na matatizo ya wananchi.

"Nimekuja na bati miambili kwa ajili ya Ujenzi wa soko tunataka kuona kila mtu anajishughulisha shughuli za uchumi," alisema.

Naomba Viongozi wa soko bati hizi zisitumike vibaya na natoa fedha kiasi cha shilingi milioni moja ili muanze kupiga ripu soko letu.

Aidha natoa shilingi milioni moja nyingine kuwapa kikundi cha hamasa, na fedha nyingine ni kwa ajili ya timu za mpira kama ilani ya Chama cha Mapinduzi inavyoeleza katika kukuza vipaji vya vijana wetu na kuwapa shilingi milioni moja nyingine vijana wa boda boda, fedha zote zitawekwa katika akaunti maalumu ya vikundi hivyo.

Waziri Mhagama amehimiza wananchi kuendelea kuchangamkia fursa za uchumi zinazojitokeza katika Halmashauri hiyo.

Katika hatua nyingine Ndg. Godfrey Mukanula aliyekuwa mmoja wa makamanda wa upinzani kutoka CDM katika Jimbo la Peramiho amejiunga na CCM.

Akizungumzia kuhusu uwaumuzi wake wa kuhama Chama Ndg. Godfrey Mukanula amesema mambo ya Maendeleo yanayofanywa na Mbunge wa Peramiho yamemhamasisha kuzaliwa katika familia upya katika Chama Cha Mapinduzi

No comments:

Post a Comment

HABARI KUU KWA SASA

"HONGERENI JKT KWA KUENDELEZA UTALII"- DC KIBAHA

  Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Mhe. Nickson Simon John amelipongeza Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kupitia kikosi chake cha Ruvu JKT kwa kuendelez...