Kura zinahesabiwa baada ya uchaguzi wa hapo jana nchini Afrika Kusini.
Mistari mirefu ilikuwa nje ya vituo vya kupigia kura kote nchini.
Afisa mmoja wa uchaguzi mjini Johannesburg aliiambia BBC kuwa misururu hiyo inakumbusha uchaguzi wa kihistoria wa 1994, wakati watu weusi walipiga kura kwa mara ya kwanza, na ambao ulishuhudia Nelson Mandela kuwa rais.
Watu wengi walikuwa bado wanangoja kupiga kura wakati kura zilipofungwa rasmi saa 2100 saa za ndani (1900 GMT) lakini tume ya uchaguzi ilisema kwamba wote wataruhusiwa kupiga kura zao.
Matokeo ya kwanza yataanza kutangazwa Alhamisi asubuhi na matokeo ya mwisho yanatarajiwa mwishoni mwajuma.
Chama cha ANC kimepoteza uungwaji mkono kutokana na hasira juu ya viwango vya juu vya rushwa, uhalifu na ukosefu wa ajira.
Kura za maoni zinaonesha kuwa huenda ikapoteza wingi wake bungeni. Sifiso Buthelezi, ambaye alipiga kura katika Joubert Park mjini.
Johannesburg, kituo kikubwa zaidi cha kupigia kura nchini Afrika Kusini, aliiambia BBC: "Uhuru ni mkubwa lakini tunahitaji kukabiliana na ufisadi."
Mabadiliko yamekuwa hisia ya mara kwa mara, hasa miongoni mwa wapiga kura vijana.
No comments:
Post a Comment