Mazungumzo ya kusitisha mapigano yaingia siku ya pili Doha huku Israel ikishambulia Ukingo wa Magharibi - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Friday, August 16, 2024

Mazungumzo ya kusitisha mapigano yaingia siku ya pili Doha huku Israel ikishambulia Ukingo wa Magharibi


Wapatanishi wa mzozo baina ya Israel na Hamas wataanza tena mkutano katika mji mkuu wa Qatar, Doha, kwa lengo la kufikia makubaliano ya mapatano katika Ukanda wa Gaza.


Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Qatar Majid Al-Ansari alisema siku ya Alhamisi kwamba mazungumzo kuhusu usitishaji mapigano na mateka huko Gaza yataendelea kwa siku ya pili mfululizo.


Msemaji huyo ameongeza katika taarifa yake kuwa juhudi za wapatanishi wa Qatar, Misri na Marekani zinaendelea, akisisitiza kuwa wapatanishi hao wamedhamiria kusonga mbele katika juhudi zao za kufikia usitishaji wa vita katika Ukanda wa Gaza ambapo mateka hao wataachiliwa huru na kiasi kikubwa zaidi cha msaada wa kibinadamu kitaingia Gaza.


Afisa wa Marekani, akizungumza na Reuters, alielezea siku ya kwanza ya mazungumzo kama "ya kujenga."


Wakati huo huo, Israel inaendelea na mashambulizi yake dhidi ya Gaza, na maafisa wa matibabu huko Gaza wanasema kuwa Wapalestina wasiopungua sita waliuawa Alhamisi jioni katika shambulio la anga la Israel kwenye nyumba moja huko Jabalia kaskazini mwa Ukanda wa Gaza.

No comments:

Post a Comment