Meneja wa Manchester United Erik ten Hag ana wasiwasi kuwa timu yake "haiko tayari" kwa mechi ya kwanza ya Ligi Kuu ya Uingereza dhidi ya Fulham siku ya Ijumaa.
Wachezaji wapya waliosajiliwa Matthijs de Ligt na Noussair Mazraoui watakuwa kwenye kikosi hicho lakini waliwasili Alhamisi.
Wamekuwa na nafasi finyu ya kufanya mazoezi na wenzao wapya, na kumwacha meneja Ten Hag na kizungumkuti cha kuchagua wachezaji 11 wa kwanza watakaomenyana na Fulham Old Trafford.
Wakati huohuo, beki Luke Shaw anauguza jeraha la mguu huku naye mlinzi mpya aliyenunuliwa kwa dau la £52m Leny Yoro akipata jeraha litakalomuweka nje kwa miezi mitatu naye fowadi Rasmus Hojlund pia akiguza jeraha la paja.
United ilijitolea kutumia karibu pauni milioni 60 kuwaleta mabeki De Ligt na Mazraoui kwenye klabu kutoka Bayern Munich.“Timu haiko tayari lakini ligi inaanza,” alisema Ten Hag.
"Kuna mameneja wengi zaidi ambao wanakabiliwa na tatizo hili lakini inabidi tuanze."Hatuwezi kujificha. Hatuwezi kuikimbia. Tunapaswa kukabiliana nayo.
"Mchezaji mwingine aliyesajiliwa na United majira ya kiangazi, mshambuliaji wa Uholanzi Joshua Zirkee, alikuwa mchezaji wa akiba ambaye hakutumika wakati wa mechi ya Ngao ya Jamii dhidi ya Manchester City na anaweza kucheza mechi yake ya kwanza dhidi ya Fulham.
Mazraoui anaweza kuwa jibu moja, huku Diogo Dalot na Lisandro Martinez wakiwa wametumika kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii Jumamosi iliyopita.
Licha ya kuwa kuna masuala kuhusu ni mchezaji gani anapaswa kuza katika kikosi cha kwanza Ten Hag bado anatarajia kupanga kikosi kikali"Sio kuhusu wachezaji ambao hawapatikani," Mholanzi huyo alisema.
"Pia ni kile nilichosema msimu uliopita - ni kuhusu wachezaji ambao wanapatikana na tuna kundi zuri, tunaweza kuchagua kikosi kikali.
"Shaw hajaichezea United tangu Februari, hasa kwa sababu ya jeraha la misuli ya paja, ingawa hatimaye alikuwa vyema kuichezea England kwenye Euro 2024.
Ten Hag ana uhakika Shaw atakuwa tayari hivi karibuni na anatazamia kurejea."Atarejea baada ya muda mfupi," Ten Hag alisema. "Haichukui muda mrefu.
No comments:
Post a Comment