Msaidizi wa karibu wa Putin Nikolai Patrushev amenukuliwa na gazeti la Urusi la Izvestia akisema kuwa Nato na nchi za Magharibi zilihusika katika kupanga uvamizi unaoendelea wa Ukraine katika eneo la Kursk, kulingana na shirika la habari la Reuters.
"Operesheni katika eneo la Kursk pia ilipangwa kwa ushirikiano wa Nato na huduma maalum za nchi za Magharibi," gazeti la Izvestia limemnukuu Patrushev.
"Taarifa za uongozi wa Marekani kwamba haikuhusika katika uhalifu wa Ukraine katika eneo la Kursk si za kweli... Bila ushiriki wao na usaidizi wa moja kwa moja, Kyiv isingeingia katika eneo la Urusi."
Mapema wiki hii, Ikulu ya Marekani ilisema kwamba haikuwa na taarifa ya mapema kuhusu operesheni hiyo na haikuhusika.
Ukraine inasema vikosi vyake vinaendelea kusonga mbele katika eneo la Urusi na pande mbalimbali. Pia imeanzisha ofisi ya kijeshi ndani ya Urusi.
No comments:
Post a Comment