MENEJA WA TRA MANYARA ALEX KATUNDU ATATUA KERO ZA WAFANYABIASHARA MAGUGU - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Saturday, September 21, 2024

MENEJA WA TRA MANYARA ALEX KATUNDU ATATUA KERO ZA WAFANYABIASHARA MAGUGU



Ferdinand Shayo ,Manyara

Meneja wa TRA Mkoa wa Manyara Alex Katundu amesikiliza na kutatua kero za Wafanyabiashara katika kata ya Magugu Wilayani Babati Mkoani Manyara ambapo ameambata na timu ya Maofisa wa TRA waliopiga kambi katika eneo la stendi ya zamani pamoja na Mnada wa Magugu kwa lengo la kutatua changamoto za kikodi na kuwawezesha wafanyabiashara kulipa malimbikizo ya madeni ya kodi kwa urahisi .

Katundu amesema kuwa wameamua kusogeza karibu huduma kwa wafanyabiashara katika maeneo yao ili waweze kupata huduma zote za TRA ikiwemo huduma za usajili ,kupata masuluhisho ya changamoto zao hapo hapo.

“Siku ya Alhamisi kila wiki itakua siku maalumu ya kusikiliza kero za wafanyabiashara na kuzitatua ,tutawafata wafanyabiashara huko huko walipo bila kulazimika kuja ofisini “ ameeleza Alex Katundu Meneja wa TRA Manyara .

Kwa upande wao wafanyabiashara akiwemo Stanley Mchome ameipongeza TRA kwa ubunifu wa kuwafata wafanyabiashara katika maeneo yao na kuwahudumia kwani italeta chachu ya kuongeza ulipaji kodi kwa hiari na kuhakikisha wafanyabiashara wanafanya kazi bila changamoto zozote.









No comments:

Post a Comment