Halmashauri ya Wilaya ya Karatu Mkoani Arusha Jumatano Novemba 20, 2024 imezindua kitabu maalum kilichoandaliwa kwa usaidizi wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania kikieleza mpango mkakati wa Halmashauri hiyo katika kuongeza ukusanyaji wa mapato.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Ndg. Juma Hokororo amewaambia wanahabari kuwa kitabu hicho kitatoa mwanga zaidi wa miaka mitano ijayo katika sekta mbalimbali za uzalishaji ikiwemo Kilimo, Utalii, Biashara pamoja na madini katika kuhakikisha kuwa makusanyo yanazidi yale ya Mwaka 2023/2024 ya zaidi ya asilimia 120.
Hokororo amenukuliwa akisema kuwa Halmashauri hiyo ya Wilaya ya Karatu iliyo lango la Hifadhi kubwa za utalii nchini Tanzania ilikuwa na mpango wa kukusanya Bilioni tano nukta tisa katika Bajeti ijayo lakini kupitia mpango huo mpya wanatarajia kukusanya zaidi na kufikia Bilioni zaidi ya saba.
No comments:
Post a Comment