Majaliwa kufungua mkutano wa biashara na uchumi Dodoma - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, November 13, 2024

Majaliwa kufungua mkutano wa biashara na uchumi Dodoma



🎈🎈Utakutanisha mataifa ya nje kujadili biashara na maendeleo ya kiuchumi


Na Mwandishi Wetu


WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa, anatarajiwa kufungua mkutano wa Tano wa Biashara na Maendeleo ya Kiuchumi (BEDC) 2024) ambao umeandaliwa na Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) utakaofanyika kuanzia tarehe 22 mkoani Dodoma.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkuu wa chuo cha CBE, Profesa Edda Lwoga, alisema lengo la mkutano huo ni kujadiliana kuhusu masuala muhimu yanayohusu biashara na maendeleo ya kiuchumi.

Alisema mkutano kama huo ulianzishwa mwaka 2020, na tangu wakati huo umejidhihirisha kuwa jukwaa muhimu la mijadala ya kibiashara na kiuchumi, likiwakutanisha washiriki kutoka sehemu mbalimbali za dunia.

“Lengo kuu la Mkutano wa Tano wa Biashara na Maendeleo ya Kiuchumi (BEDC 2024) ni kuwaleta pamoja wataalamu, wajasiriamali, watafiti, na wadau wa maendeleo kutoka sehemu mbalimbali za dunia kujadili masuala muhimu ya biashara na maendeleo ya kiuchumi,” alisema na kuongeza.

“Mkutano huu utajadili mbinu za kukuza biashara, masuala ya uwekezaji, uvumbuzi, maendeleo endelevu, na changamoto za kiuchumi, huku ukitoa fursa ya kubadilishana mawazo, kujifunza, na kujenga mtandao wa kitaalamu kwa ajili ya maendeleo ya uchumi wa dunia,” alisema.

Alisema mkutano huo unatoa fursa muhimu kwa washiriki kupata maarifa mapya, kujenga mitandao ya kitaalamu, na kuchangia katika maendeleo endelevu ya biashara na uchumi duniani.

“Tunakaribisha wataalamu, wajasiriamali, na wadau wa maendeleo kushiriki katika mkutano huu ili kujadiliana na kuboresha sekta mbalimbali za uchumi na biashara duniani,” alisema.

Alisema makongamano hayo yalianza mwaka 2016 mara baada ya serikali kutangaza kuhamia Dodoma na baadaye yakageuka kuwa mikutano ya kitaaluma, yakilenga kuimarisha mijadala na tafiti zinazohusu biashara na maendeleo ya kiuchumi.

Alisema mikutano hiyo imekuwa ikikusanya wataalamu, wafanyabiashara, na wadau wa maendeleo kutoka ndani na nje ya nchi ili kujadili na kubadilishana mawazo, kutoa mapendekezo, na kuhamasisha ushirikiano kwa ajili ya maendeleo endelevu.

“Napenda kuwafahamisha kuwa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) kinapenda kuwajulisha wote kuwa Kongamano la tano la Maendeleo ya Biashara na Uchumi 2024 litafanyika tarehe 22 - 23 Novemba, 2024 katika Ukumbi wa Mikutano wa Treasury squire jijini Dodoma. Mkutano huu una kauli mbiu ya : “Business Environment and Trade Facilitation For The Inclusive Development” kwa kiswahili ni" Mazingira ya Biashara na Urahisishaji wa Biashara kwa Maendeleo Jumuishi ".

Alisema tangu mwaka 2020, Chuo kimeandaa mikutano minne ya kitaaluma, ambayo yote imelenga kuunga mkono juhudi za serikali za kukuza fursa za biashara na uwekezaji nchini.

Alisema katika mkutano wa BEDC wa mwaka 2022/2023, jumla ya machapisho 169 na matokeo ya tafiti ziliwasilishwa na watafiti kutoka ndani na nje ya nchi na kujadiliwa na wataalamu mahiri katika fani mbalimbali.

Alisema mawasilisho katika Kongamano hilo yatajikita katika mada ndogo ambazo zitajadiliwa baada ya ufunguzi na mawasilisho ya wasemaji muhimu na kwamba mwaka huu CBE inatarajia kutakuwa na machapisho zaidi ya 170 yatakayolenga katika mada ndogo saba na kwamba watoa mada wanaotarajiwa wanatoka nchi za Afrika Mashariki, Ethiopia, na China.

Alitaja malengo makuu ya mkutano wa mwaka huu kuwa ni pamoja na kujenga uwezo na mitandao, kukuza maarifa, kuunda mitandao, fursa za kibiashara, kutangaza kazi za wataalamu na fursa za maendeleo ya kiuchumi.

No comments:

Post a Comment