RAIS DKT. SAMIA : KILICHOPO KWENYE BOKSI NDICHO KITAKACHO TANGAZWA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, November 27, 2024

RAIS DKT. SAMIA : KILICHOPO KWENYE BOKSI NDICHO KITAKACHO TANGAZWA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluh Hassan ameshiriki zoezi la upigaji kura leo Novemba 27,2024 katika kituo Cha sokoine kijiji cha Chamwino Ikulu Mkoani Dodoma.

Ikumbukwe kuwa Oktoba 11,2024 ndicho Kituo alichojiandikisha Rais Samia kwenye daftari la kudumu la mpiga kura ili kupata nafasi ya kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaondelea leo Novemba 27,2024 nchini kote.

Akizungumza Mara baada ya kukamilisha zoezi hilo Rais Dkt. Samia amewataka Watanzania kuchagua viongozi wenye sifa za kuongoza , wapige kura kwa maelewano pamoja kuendelea kulinda usalama na kutunza amani ya nchi.

Aidha, Rais Dkt. Samia amewataka Wasimamizi wa Uchaguzi huo kutangaza matokeo kulingana na kura zilizopigwa.





No comments:

Post a Comment