WAZIRI wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) , Dk. Stergomena Tax leo tarehe 27 Novemba 2024 ameshiriki zoezi la uchaguzi wa viongozi wa serikali za mitaa katika kituo cha Unyamwezini kata ya itumbili wilayani Magu mkoani Mwanza na kuwataka wananchi kutumia fursa hiyo kuchagua viongozi wanaoona wana uwezo kuwaongoza.
Waziri Tax ambaye ni mkazi wa Magu ametoa wito kwa wananchi wote kufika kwenye vituo vilivyoandaliwa ili wapige kura na muhimu wachague viongozi ambao wanaridhika nao.
“Mara nyingi hatuendi kuchagua viongozi baada ya hapo wakishachaguliwa tunaanza kulalamika, basi kama Rais Samia Suluhu Hassan alivyotuhamasisha wote akasema tusipoteze fursa hii… tuitumie fursa hii kuchagua viongozi ambao watatuletea maendeleo na kudumisha amani na usalama.
“Tuende kupiga kura kuchagua viongozi ambao tunaona wanatufaa lakini pia tutekeleze wajibu wetu na haki yetu ya kikatiba,” amesema.
No comments:
Post a Comment