Na Mwandishi wetu.
Mwenyekiti wa kitongoji cha Mwangida Kaskazini Mkoani Kigoma kutoka Chama cha ADC ambaye pia ni mkurugenzi wa uchaguzi wa Chama hicho Taifa Ndg. Mtoro Bakar Mvunye ambaye amechaguliwa Novemba 27 katika uchaguzi wa serikali za mitaa, vijiji na Vitongoji nchini ameshangaa kutembelewa na kiongozi wa CCM baada ya kuwashinda katikq uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
Amesema jambo kubwa katika kuwaletea maendeleo wananchi ni kushirikiana na kwa kuwa CCM iko tayari na haina kinyongo na ushindi wa upinzani anaamini kitongoji chake na vingine ambavyo wananchi wamefanya uchaguzi na kuchagua upinzani vitapata maendeleo.
Amesema kuwa pamoja na kwamba ameshinda uchaguzi, lakini alikuwa anawaza anamfikishiaje diwani na mbunge wa CCM matatizo ya wananchi wake, lakini sasa anauona mwanga wa kazi kwani itakuwa nyepesi na atateua wajumbe wa kumsaidia kutoka vyama vyote alivyogombea navyo ili tushirikiane katika uongozi" alisema Mvunye.
Kwa upande wake Katibu wa siasa,uenezi na mafunzo wa Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Kigoma Deogratius Nsokolo amemtembelea katika kitongoji chake cha mwangida kaskazini katika wilaya ya Kigoma Mkoani Kigoma mwenyekiti wa kitongoji hicho kutoka Chama cha ADC ambaye pia ni mkurugenzi wa uchaguzi wa Chama hicho Taifa Ndg. Mtoro Bakar Mvunye ambaye amechaguliwa Novemba 27 katika uchaguzi wa serikali za mitaa, vijiji na Vitongoji nchini.
Nsokolo amesema amefika katika mtaa huo ili kumpongeza mwenyekiti huyo kwa ushindi ikiwa ni mgombea pekee wa chama hicho aliyeibuka mshindi, lkn pia ni kiongozi wa kitaifa wa Chama hicho akiwa mkurugenzi wa uchaguzi wa ADC Taifa.
Katika mazungumzo yao Katibu Mwenezi wa Mkoa amemuhakikishia ushirikiano kutoka chama cha Mapinduzi na Serikali katika kuwahudumia wananchi , kulinda usalama wa raia, kusimamia maendeleo ya wananchi, kudumisha upendo na mshikamano na kuwaunganisha wananchi kuwa kitu kimoja.
Amesema mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi anasisitiza juu ya mambo manne ambayo ni Maridhiano, ustahimilivu ,mabadiliko na kujenga upya, hivyo CCM katika mkoa wa Kigoma inayaishi mambo hayo ili kuwafanya Wananchi washirikiane katika maendeleo bila kujali itikadi zao za vyama na kwamba CCM itaendelea kushirikiana na viongozi wote waliochaguliwa kupitia vyama mbalimbali vya siasa.
No comments:
Post a Comment