Na Mwandishi Wetu, Dodoma
Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), inaendelea kutekeleza Mpango Kabambe wa Maendeleo ya Bandari (2020 – 2045) pamoja na programu ya uboreshaji na uendeshaji wa bandari, ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kitaifa.
Hayo yameelezwa leo Februari 24,2025 na Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Plasduce Mbossa, wakati akitoa taarifa ya mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan katika kipindi cha miaka minne ndani ya sekta ya Bandari.
Mbossa amesema mpango huo unahusisha miradi 10 ya kimkakati inayolenga kuimarisha bandari na kuongeza ufanisi wake, ambapo amesema Miongoni mwa miradi hiyo ni pamoja na ujenzi wa Mradi wa kupokelea na kuhifadhia mafuta – ambao Unagharimu dola za kimarekani milioni 265, na utekelezaji wake umefikia asilimia 17. Ukikamilika, utapunguza muda wa kuhudumia meli zenye ujazo wa 150,000 DWT kutoka siku 10 hadi siku 3.
Pili, Ujenzi wa kituo cha reli na mtandao wake ndani ya bandari ya Dar es Salaam – Utagharimu dola milioni 119.9 na utapunguza shehena inayosafirishwa kwa barabara kwa asilimia 98, hivyo kupunguza msongamano wa malori bandarini.
Tatu, Ujenzi wa gati mbili zenye urefu wa mita 500 – Gharama ya dola milioni 250, zikikamilika zitawezesha meli mbili kubwa za 50,000 DWT kutia nanga kwa wakati mmoja.
Nne, Ujenzi wa bandari maalum ya Kisiwa – Mgao (Mtwara) – Unagharimu dola milioni 171, ukilenga kuhudumia shehena chafu na kupunguza athari za kimazingira katika bandari ya Mtwara.
Tano, Uboreshaji wa gati namba 8 – 11 na maeneo ya kuhifadhia makasha – Unagharimu dola milioni 220.
Sita, Uendelezaji wa bandari kavu Kurasini na Ihumwa – Dodoma – Utagharimu dola milioni 157.
Saba, Uboreshaji wa bandari ya Kigoma – Unagharimu dola milioni 48.82, ukilenga kuimarisha biashara katika ushoroba wa kati.
Nane, Ujenzi wa gati maalum la kuhudumia makasha na gati la mafuta – Bandari ya Tanga – Utagharimu dola milioni 201.
Tisa, Ujenzi wa gati namba 12 – 15 katika bandari ya Dar es Salaam – Utagharimu dola milioni 591.564, ukilenga kuongeza ufanisi wa bandari.
Kumi, Ujenzi wa bandari mpya ya Mbegani – Bagamoyo – Mradi mkubwa unaogharimu dola bilioni 1.5, ambao utachochea ukuaji wa sekta ya bandari nchini.
Miradi hiyo inalenga kuimarisha miundombinu ya bandari, kuongeza ufanisi wa usafirishaji na kuchochea ukuaji wa uchumi wa taifa.

No comments:
Post a Comment