SERIKALI YAWAHIMIZA WANANCHI KUMNADI NA KUMUOMBEA PROF. MOHAMED JANABI KATIKA UCHAGUZI WA MKURUGENZI WA WHO KANDA YA AFRIKA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Saturday, March 22, 2025

SERIKALI YAWAHIMIZA WANANCHI KUMNADI NA KUMUOMBEA PROF. MOHAMED JANABI KATIKA UCHAGUZI WA MKURUGENZI WA WHO KANDA YA AFRIKA




Na Okuly Julius _DODOMA


Serikali imetoa wito kwa wananchi wote kumnadi na kumuombea Mgombea wa nafasi ya Ukurugenzi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Kanda ya Afrika P
Profesa Mohamed Janabi ili ashinde nafasi hiyo.

Kauli hiyo imetolewa leo Machi 22,2025 jijini Dodoma na Waziri wa Afya Mhe. Jenista Mhagama wakati akimtambulisha Mgombea wa nafasi ya Ukurugenzi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Kanda ya Afrika Profesa Mohamed Janabi

"Kampeni za wagombea wa nafasi hii tayari zimeshaanza kwa njia mbalimbali, nasi hatuna budi kushirikiana kumnadi mgombea wetu kwa nguvu, ari na morari kubwa. Nitoe rai kwa wananchi, mashirika na wadau wa Sekta wa ndani na nje kuungana pamoja katika kumnadi na kumuombea dua mgombea wetu, " amesisitiza Mhagama

Waziri Mhagama amesema kutokana na kukua kwa kasi kwa mahusiano mazuri ya Kidiplomasia pamoja na ushirikiano ambao Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameendelea kuimirisha baina ya nchi ya Tanzania na Mataifa mengine, jambo hilo linaipaisha Tanzania kwenye majukwaa ya Kikanda na Kimataifa.

"Taifa letu lina sifa ya kutoa viongozi wenye weledi katika nyanja mbalimbali, na tunajivunia kwamba Prof. Janabi yuko tayari kulihudumia Bara letu katika nafasi hii kwa ustadi wa hali ya juu,"

Na kuongeza "uzoefu wa Prof. Janabi katika masuala ya ugharamiaji wa huduma za afya kwa kuzingatia kipindi hiki ambacho Dunia inapita katika changamoto ya kubuni vyanzo vya uhakika katika ugharamiaji wa huduma za afya na uzalishaji wa bidhaa za afya nchini pamoja na usimamiaji wa mifumo ya utoaji wa huduma za afya zinatupa nafasi kubwa ya kushinda nafasi hii, "amesema Mhagama

Vilevile, Mhagama amesena uzoefu wake umedhihirika katika kuzuia, kudhibiti na kupambana na magonjwa ya mlipuko pamoja na magonjwa yasiyoambukiza ambayo yamekuwa yakiongezeka kwa kasi kubwa ulimwenguni.

Waziri Mhagama ameezea imani kubwa iliyopo juu ya Prof. Janabi
Katika nafasi hiyo kwani ameshafanya Mapinduzi makubwa katika sekta ya Afya ndani ya nchi na nje ya nchi.

"Tuna imani kuwa kwa uongozi wake, Afrika itapiga hatua kubwa katika kuboresha mifumo ya afya, kupambana na magonjwa, na kuhakikisha kila mwananchi anapata huduma bora za afya," amesema Mhagama

Mkurugenzi wa Kanda anachaguliwa kwa kura ya siri katika kikao cha ndani cha Kamati ya Kanda ya WHO kwa Afrika, ambayo ilikutana Januari 14, 2025, na kuamua kutumia utaratibu wa haraka, kumpata Mkurugenzi wa Kanda badala ya mchakato wa kawaida ambayo huchukua muda mrefu na uchaguzi huo unatarajiwa kufanyika Mei 18, 2025.

Ikumbukwe kuwa Prof. Janabi anaingia katika uchaguzi huo akishindana na wagombea wengine watatu ambao ni: Profesa Moustafa Mijiyawa (Togo), Dkt. Michael Yao (Ivory Coast) na Dr. Mohamed Lamine Drame (Guinea Conakry) ili kuziba nafasi ya aliyekuwa Mkurugenzi Mteule wa Kanda hiyo, Dk. Faustine Ndugulile, waziri wa wa zamani wa afya Tanzania, aliyefariki ghafla Novemba 2024.






No comments:

Post a Comment