🎈🎈Waziri wa Mambo Nje Misri atembelea Bwawa la Julius Nyerere
🎈🎈Asifu hatua za Rais wa Tanzania na Misri kusimamia utekelezaji wa mradi
🎈🎈Mradi wafikia asilimia 99.89
Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Judith Kapinga, amesema Tanzania na
Misri zitaendeleza ushirikiano kwenye utekelezaji wa miradi ya umeme
na kudunisha ushirikiano uliowekwa na waasisi wa nchi hizo.
Mhe Kapinga ameyasema hayo leo tarehe 20 Machi,2025, mkoani Pwani
wakati alipofanya ziara katika mradi wa umeme wa Julius Nyerere
(JNHPP) pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje, Uhamiaji na Wamisri waishio
nje ya Jamhuri ya Misri, Dkt Badir Abdelatty ikiwa ni sehemu ya ziara
ya kikazi ya Waziri Badir na ujumbe wake.
‘’ Tunamshukuru sana Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwani amekuwa
msingi imara wa utekelezaji wa miradi huu wa umeme na tumeona
matunda halisi ya usimamizi wake.’’ Amsema Mhe.Kapinga
Amesema nchi ya Misri imetekeleza mradi huo wa JNHPP kwa kuzingatia
matakwa ya nchi ya Tanzania ambapo mpaka sasa mashine nane kati ya
tisa zimewashwa na kuingizwa kwenye gridi ya Taifa
Akizungumza mara baada ya kutembelea na kujionea maendeleo ya mradi wa
JNHPP, Waziri, Dkt Badir Abdelatty, amesifu ushirikiano wa muda mrefu
uliopo kati ya Tanzania na Misri na kuishukuru Tanzania kwa kuiamini
nchi yake kutekeleza mradi huo wa JNHPP, kwani utawanufaisha wananchi
wa Tanzania walio wengi hususani wale wanaozungukwa na eneo la mradi.
Amesema nchi za Afrika zinapaswa kujivunia uwepo wa miradi ya umeme
kwa maendeleo ya waafrika wenyewe na kuahidi kuwa Misri itaendeleza
ushirikiano na Tanzania kwenye utekelezaji wa miradi mingine kama hiyo
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Mambo ya Nje anayeshughulikia
masuala ya Afrika Mashariki Mhe Dannis Londo amesema, Tanzania na
Misri zitaendeleza ushirikiano wa kidiplomasia ulionao ili kufungua
fursa mbalimbali za kiuchumi hususani kwenye miradi ya sekta ya
Nishati
Ziara hiyo.imehudhuriwa na Balozi wa Tanzania nchini Misri, Balozi wa
Misri nchini Tanzania, Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Mafuta, Dk
James Mataragio, na viongozi mbalimbali kutoka Wizara ya Nishati na
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Cap
Naibu Waziri wa Nishati, Mhe Judith Kapinga ( wan ne kushoto) akiwa
katika kwenye mradi wa umeme wa Julius Nyerere (JNHPP) pamoja na
Waziri wa Mambo ya Nje, Uhamiaji na Wamisri waishio nje ya Jamhuri ya
Misri, Dkt Badir Abdelatty ( wan ne kulia) tarehe 20 Machi 2025. Wa
tatu kulia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje anayeshughulikia masuala
ya Afrika Mashariki Mhe Dannis Londo
No comments:
Post a Comment