MAPATO YATOKANAYO NA SEKTA YA UTALII YAPAA - BALOZI DKT. CHANA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Monday, May 19, 2025

MAPATO YATOKANAYO NA SEKTA YA UTALII YAPAA - BALOZI DKT. CHANA



Na Okuly Julius DODOMA


Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana, amesema kuwa mapato yatokanayo na shughuli za utalii yameongezeka kwa kiwango kikubwa katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita.

Amesema mapato kutoka kwa watalii wa kimataifa yameongezeka kutoka Dola za Marekani bilioni 1.3 mwaka 2021 hadi Dola za Marekani bilioni 3.9 mwaka 2024, sawa na ongezeko la asilimia 200.

Wazira Chana ameyasema hayo leo Mei 19,2025 Bungeni jijini Dodoma wakati akiwasilisha Hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2025-2026.

Aidha, mapato yatokanayo na utalii wa ndani yamepanda kutoka Shilingi bilioni 46.3 mwaka 2021 hadi Shilingi bilioni 209.8 mwaka 2024, ikiwa ni ongezeko la asilimia 353.1.

Kwa mujibu wa Waziri Chana, mafanikio hayo yameiwezesha Tanzania kushika nafasi ya tisa (9) duniani na nafasi ya tatu (3) barani Afrika kwa ongezeko la mapato ya utalii, ikilinganishwa na hali ilivyokuwa kabla ya janga la UVIKO-19.

No comments:

Post a Comment