
Mwanzilishi na Afisa Mtendaji Mkuu wa WazoHuru Media Group Limited Ndg Mathias Canal ameshinda Tuzo mbili za SAMIA KALAMU AWARDS sekta ya Ujenzi na chombo bora cha mtandaoni.
Pamoja na zawadi ya Cheti, Ngao, Tsh Milioni 10, lakini pia Mathias Canal amezawadiwa safari ya kwenda nchini Japani pamoja na kufanya kazi ya kusafiri nchi nzima kueleza kwenye vyombo vya habari mafanikio na utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 2020-2025.
Tuzo hizo zimetolewa leo tarehe 5 Mei 2025 katika ukumbi wa Super Dome Masaki Jijini Dar es salaam ambapo mgeni rasmi katika tukio hilo alikuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan
Tuzo hizo zimetolewa kwa wanahabari watanzania kwa lengo la kuhamasisha, kuhimiza na kukuza wigo wa uchakataji, utangazaji na uchapishaji wa maudhui ya ndani kupitia vyombo vya habari.
Tuzo hizi zitahusisha maudhui yaliyochapishwa kupitia magazeti, redio, televisheni, majukwaa ya mtandaoni pamoja na tuzo kwenda kwa vyombo vya habari. Tuzo hizi zinahusisha habari zilizochapishwa kati ya Januari 01 hadi Oktoba 26, 2024.
Akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi Mhe Abdalah Ulega, Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe Innocent Bashungwa (Mb) amesema kuwa pamoja na zawadi ya Tuzo pia Waziri Ulega amempa zawadi ya kufanya kazi katika wizara hiyo hivyo akaripoti Wizarani kwa ajili ya kuanza kazi.
No comments:
Post a Comment