MKONGO WA TAIFA WAUNGANISHA WILAYA 109, SERIKALI YASONGA MBELE KWA KADI JAMII - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, May 15, 2025

MKONGO WA TAIFA WAUNGANISHA WILAYA 109, SERIKALI YASONGA MBELE KWA KADI JAMII



Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Jerry Slaa amesema Mkongo wa Taifa unaosimamiwa na Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) umeshaunganisha wilaya 109 kati ya 139, na kazi inaendelea ili kufikia wilaya zote 139 nchini. Aidha, baadhi ya nchi za Afrika tayari zimeunganishwa na mkongo huo, hatua inayoongeza ufanisi wa huduma za mawasiliano na mifumo ya kidijitali barani Afrika.

Katika hatua nyingine, Serikali inaendelea na mchakato wa kurahisisha malipo kwa kutumia kadi moja ya Kadi Jamii, ambayo itaunganishwa na huduma mbalimbali za malipo zikiwemo taasisi za kifedha, viingilio vya viwanja vya mpira, malipo ya vivuko, huduma za UDART na mengineyo.

Akizungumza baada ziara ya Mhe. Kassim Majaliwa(Mb), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, alipotembelea Kituo cha Kuhifadhi Data Kimtandao (NIDC) kwa lengo la kuangalia Mfum wa N- CARD unavyofanya kazi,Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Jerry Slaa, alisema Serikali imejipanga kuhakikisha mifumo yote inasomana kwa lengo la kuimarisha utoaji wa huduma kwa wananchi kupitia Mradi wa Digital Tanzania.

Alibainisha kuwa kupitia mradi huo, taasisi za umma na binafsi haziitaji tena kuwekeza kwenye mifumo yao binafsi, bali zitatumia huduma za NIDC kwa gharama nafuu na usalama wa kuaminika.

“Katika bajeti ya mwaka 2024/2025, Serikali ilitenga Shilingi bilioni 10 kuiwezesha NIDC kutekeleza huduma zake, ikiwa ni pamoja na utekelezaji wa Mradi wa Digital Tanzania,” alisema Waziri Slaa.

Alifafanua kuwa kupitia mradi huo, wananchi wataunganishwa kupitia namba zao za NIDA na kupewa Kadi Jamii itakayowawezesha kufanya miamala yote ya kifedha na manunuzi kwa urahisi, hivyo kupunguza haja ya kuwa na kadi nyingi za huduma mbalimbali.

Serikali pia ina mpango wa kuhakikisha kila mwananchi anapata kadi janja kwa kupunguza gharama za simu janja zitakazotumika kwa mfumo huo, ikiwa ni sehemu ya kuhakikisha ushirikishwaji wa kila mmoja katika mapinduzi ya kidijitali.

No comments:

Post a Comment