Na Okuly Julius DODOMA
Waziri wa Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa ameanisha vipaumbele vya wizara hiyo katika mwaka wa fedha 2025/26, ikiwemo kuendelea na ujenzi wa Reli ya Kisasa ya SGR (Standard Gauge Railway) katika Ushoroba wa Kati
Waziri Mbarawa ametoa kauli hiyo leo Mei 15, 2025, Bungeni jijini Dodoma, wakati akitoa hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Uchukuzi kwa mwaka wa fedha 2025/2026.
"Wizara ya Uchukuzi itaendelea kutekeleza majukumu yake kwa kuzingatia vipaumbele vilivyolenga kuimarisha utoaji wa huduma za uchukuzi nchini,"amesema Profesa Mbarawa
Vipaumbele Vingine ni pamoja na kuendelea kuboresha miundombinu ya reli ya TRC (Metre Gauge Railway - MGR) na reli ya TAZARA (Cape Gauge Railway - CGR), ikiwemo kipande cha kutoka Kilosa hadi Kidatu (km 108) kwa ajili ya kuunganishwa na reli ya TAZARA,kuendelea kuboresha Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL);
Pamoja na kuendelea na ununuzi na ukarabati wa vitendea kazi, ikiwemo vichwa vya treni, mabehewa na mitambo ya ukaguzi wa reli,kuboresha miundombinu na huduma katika Bandari za Bahari na Maziwa Makuu,Kuendelea na ujenzi wa bandari kavu nchini, ikiwemo Bandari Kavu ya Kwala ambayo inalengwa kuwa bandari ya kimkakati.
"Kuimarisha usalama na mawasiliano kwenye usafiri na usafirishaji katika Maziwa Makuu nchini,Uendelezaji na uendeshaji wa viwanja vya ndege,Kuimarisha usalama na kudhibiti uchafuzi wa mazingira katika usafiri wa anga, ardhini na majini na Kuendelea na ujenzi wa meli mpya na ukarabati wa meli zilizopo kwa ajili ya kubeba abiria na mizigo katika Maziwa Makuu pamoja na Kuimarisha huduma za usafiri na usafirishaji majini,"Profesa Mbarawa
Pia Profesa Mbarawa amesema wizara hiyo itaendelea kuwajengea uwezo watumishi wa Wizara na kuboresha mazingira ya kazi ili kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma za uchukuzi,Kutekeleza mikakati ya upatikanaji wa mizigo kwa ajili ya reli ya SGR na kuanza kutoa huduma ya usafirishaji mizigo kwa hatua za awali,Kuendelea kuboresha mifumo ya TEHAMA kwa ajili ya kuongeza ufanisi wa utoajihuduma,Kuimarisha ufuatiliaji na tathmini ya miradi na shughuli za Wizara.
No comments:
Post a Comment