WATUMISHI WIZARA YA FEDHA WAJIVUNIA UTALII WA NDANI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Sunday, May 11, 2025

WATUMISHI WIZARA YA FEDHA WAJIVUNIA UTALII WA NDANI



Na. Saidina Msangi na Scola Malinga, WF, Dar es Salaam.


Watumishi wa Wizara ya Fedha wakiongozwa na Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Rasilimali Watu Bw. Lusius Mwenda, wametembelea Kituo cha Kihistoria cha Magofu ya Kaole, Bagamoyo mkoani Pwani kujionea vivutio vya utalii vilivyoko eneo hilo.

Watumishi hao wamefanya utalii wa ndani ikiwa ni sehemu ya Mkutano wa 38 wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Fedha, ambao umekutanisha Wajumbe kutoka Makao Makuu ya Wizara, Wakuu wa Hazina Ndogo na Wahakikimali kutoka Mikoa yote ya Tanzania Bara.

Mkutano huo ni mwendelezo wa mikutano mingine ambayo imekuwa ikifanyika kila mwaka ambapo kupitia mikutano hiyo wajumbe wamekuwa wakitoa maoni na mapendekezo ambayo yamesaidia kwa kiasi kikubwa kuboresha maslahi ya watumishi na utendaji kazi wa Wizara.










No comments:

Post a Comment