Msimamizi wa Mafunzo na Maendeleo wa Barrick nchini, Elly Shimbi (kushoto) akimpongeza mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mkwawa,Mussa Constantine baada ya kumkabidhi cheti cha ushiriki wa kongamano hilo,wengine pichani ni Afisa Uhusiano wa Chuo Kikuu cha Iringa,Fanleck John, wa pili kutoka kulia ni Rais wa AIESEC Vicent Manira na Waziri Mkuu wa Serikali ya Wanafunzi Chuo Kikuu cha Mkwawa,Doto Busagara.
Msimamizi wa Mafunzo na Maendeleo wa Barrick nchini, Elly Shimbi akiongea katika kongamano hilo.
Baadhi wa washiriki wa kongamano hilo wakifuatilia mada mbalimbali
Baadhi wa washiriki wa kongamano hilo wakifuatilia mada mbalimbali
Baadhi wa washiriki wa kongamano hilo wakifuatilia mada mbalimbali
Baadhi ya washiriki wakifurahi wakicheza kwa furaha wakiwa na vipeperushi vya Barrick ambayo imedhamini kongamano hilo
Baadhi ya Washiriki katika picha ya pamoja na watoa mada na wadhamini waliokuwa wamekaa meza kuu.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Barrick katika kongamano hilo.
**
Vijana wasomi nchini waliopo vyuoni wametakiwa kuongeza bidii, maarifa katika masomo yao na kuwa wabunifu ili kuweza kupenya kwenye soko la ajira kwenye taasisi mbalimbali ikiwemo migodini sambamba na kuweza kujiajiri kwa kutumia taaluma zao pindi wamalizapo masomo sambamba na kuchangamkia fursa muhimu kwa mafanikio ya kitaaluma.
Ushauri huo umetolewa na , Msimamizi wa Mafunzo na Maendeleo wa Barrick, Elly Shimbi, wakati akieleza shughuli za kampuni na program zake wezeshi kwa jamii kwa Wanafunzi wa vyuo vikuu vilivyopo mkoani Iringa katika kongamano lililoandaliwa na taasisi ya kuchipua na kuendeleza vipaji kwa vijana ya AIESEC Tanzania ambalo limedhaminiwa na Barrick nchini kwa kushirikiana na taasisi mbalimbali ambalo limefanyika katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Iringa.
Alisema Barrick nchini ambayo inaendesha shughuli zake kwa ubia na Serikali ya Tanzania kupitia kampuni ya Twiga Minerals, itaendelea kutafuta rasilimali watu kwa ajili ya kufanya kazi kwenye migodi yake ikiwemo vijana wanaohitimu kutoka kwenye vyuo vikuu mbalimbali na vya ufundi vya kati hapa nchini na lengo kubwa kuhakikisha inaendelea kuibua vipaji na kuunga mkono jitihada za Serikali za kupunguza changamoto ya ukosefu wa ajira.
“Ni muhimu kwa vijana wasomi kukuza utamaduni kwa kushirikiana na kuwasiliana kwa karibu (networking) katika juhudi za kusaka ajira na kutafuta fursa mbalimbali za kuwakwamua kimaisha ili kuleta matokeo Chanya kwenye jamii,” aliongeza Shimbi.
Bw. Shimbi, aliwaeleza washiriki kuwa migodi inayomilikiwa na Barrick nchini ya North Mara na Bulyanhulu imekuwa ikitoa fursa kwa vijana wa vyuo vikuu kuomba ajira mara tu wanapomaliza masomo na wakiwa kazini wanapata nafasi ya kujengewa uwezo na kampuni pia kampuni inayo programu ya kutoa nafasi ya mafunzo kwa vitendo kwa Wanafunzi wanapokuwa bado wako vyuoni.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa AIESEC Tanzania, Vicent Manira, alisema kuwa mapinduzi ya teknolojia yamesukuma mabadiliko makubwa kwenye sekta ya ajira ambapo ubunifu na ujuzi kuhusu sayansi na teknolojia ni muhimu kwa vijana ili kuweza kuingia soko la ushindani wa ajira hapa nchini sambamba na kuibua fursa za kujiajiri.
''Hivi sasa tupo kwenye kipindi ambacho kunatokea mabadiliko ya sayansi na teknolojia siku hadi siku,ili kutobaki nyuma ni muhimu kusoma kwa bidii sambamba na kufuatilia mabadiliko yanayojitokeza na kuathiri kila fani vilevile kuwa wabunifu",alisema Manira.
Baadhi ya washiriki wa kongamano hilo wameipongeza kampuni ya Barrick nchini kwa kufanikisha wanafunzi kujengewa uwezo kupitia udhamini wa semina za kuwajenga kitaaluma wanafunzi zinazoandaliwa na AIESEC Tanzania kila mwaka.
"Tunaipongeza Barrick kwa kuwezesha Wanafunzi wa vyuo vikuu vilivyopo mkoani Iringa kwani tumeweza kujifunza mengi kuhusu fursa mbalimbali zilizopo na jinsi ya kuzichangamkia", alisema Mussa Constantine kutoka Chuo Kikuu cha Mkwawa kwa niaba ya wenzake.
Semina za kuwanoa vijana wasomi vyuoni kupitia taasisi ya AIESEC kwa udhamini wa Barrick nchini mwaka huu tayari zimefanyika katika mikoa ya Dar es Salaam, Morogoro, Dodoma na Zanzibar.
No comments:
Post a Comment