WALIMU WANAWAKE KONDOA WAMZAWADIA TUZO DC FATMA KWA UONGOZI MAHIRI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Sunday, June 1, 2025

WALIMU WANAWAKE KONDOA WAMZAWADIA TUZO DC FATMA KWA UONGOZI MAHIRI



Walimu wa Wilaya ya Kondoa wamempa tuzo ya heshima Mkuu wa Wilaya Kondoa Mhe. Fatma Almasi Nyangasa kwa kuongoza wilaya kwa umahiri na kumuwakilisha vyema Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Tuzo hiyo imetolewa katika uwanja wa Puma baada ya kukamilisha mapokezi ya maandamano ya kihistoria ya wanawake wa wilaya ya Kondoa yaliyofanyika kwa lengo la kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan

Aidha walimu hao wakiongozwa na Mwenyekiti wa CWT Kondoa Mwalimu Esther Ntomola amesema wanatoa tuzo hiyo kwa Mhe. Mkuu wa Wilaya kwa kuwa kinara katika uongozi wake na kuwa karibu na wananchi na watumishi.

Maandamano ya wanawake Kondoa wamewakutanisha wanawake zaidi ya 2000 kutoka ndani ya wilaya ya Kondoa wakiwemo watumishi na wananchi.



No comments:

Post a Comment