DKT. ASHATU KIJAJI ACHUKUA NA KUREJESHA FOMU YA KUGOMBEA UBUNGE KONDOA KWA TIKETI YA CCM - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Sunday, June 29, 2025

DKT. ASHATU KIJAJI ACHUKUA NA KUREJESHA FOMU YA KUGOMBEA UBUNGE KONDOA KWA TIKETI YA CCM



Mbunge wa Jimbo la Kondoa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji, leo amechukua na kurejesha fomu ya kuomba ridhaa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na wananchi ili kuwania tena nafasi ya Ubunge wa Jimbo hilo katika uchaguzi ujao.

Fomu hiyo ameichukua na kuirejesha katika Ofisi za CCM Wilaya ya Kondoa, ambapo ilipokelewa rasmi na Kaimu Katibu wa CCM Wilaya ya Kondoa, Ndugu Juma Seif.

Akizungumza mara baada ya kurejesha fomu, Dkt. Kijaji alieleza kuwa ameamua kugombea tena nafasi hiyo kutokana na mafanikio yaliyopatikana katika kipindi cha uongozi wake, hususan katika sekta ya elimu. Alitaja baadhi ya mafanikio hayo kuwa ni pamoja na ujenzi wa shule mpya, mabweni, na upatikanaji wa vifaa vya kujifunzia katika shule mbalimbali ndani ya jimbo hilo.

No comments:

Post a Comment