
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba akiagana na Kiongozi Mwakilishi wa Benki ya Dunia, Bi. Abha Prasad, baada ya kumalizika kwa kikao kazi kuhusu ushirikiano wa kimaendeleo kati ya Tanzania na Benki hiyo, kikao hicho kilifanyika katika Ofisi za Wizara ya Fedha, Treasury Square, jijini Dodoma.

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, akizungumza na Timu ya Benki ya Dunia kuhusu ushirikiano wa kimaendeleo kati ya Tanzania na Benki hiyo, kikao hicho kilifanyika katika Ofisi za Wizara ya Fedha, Treasury Square, jijini Dodoma.

Kiongozi wa Mpango wa Ukuaji wa Usawa, Fedha na Taasisi, kutoka Benki ya Dunia, Bi. Abha Prasad, akizungumza na Timu ya wataalam ya Wizara ya Fedha katika kikao kazi kuhusu ushirikiano wa kimaendeleo kati ya Tanzania na Benki hiyo, kikao hicho kilichofanyika katika Ofisi za Wizara ya Fedha, Treasury Square, jijini Dodoma.

Kamishna wa Idara Usimamizi wa Deni la Serikali, Wizara ya Fedha, Bw. Japhet Justine akizungumza na Timu ya Wataalam kutoka Benki ya Dunia nchini Tanzania kuhusu ushirikiano wa kimaendeleo kati ya Tanzania na Benki hiyo, kikao hicho kilifanyika katika Ofisi za Wizara ya Fedha, Treasury Square, jijini Dodoma.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Dodoma)
Na Chedaiwe Msuya, WF, Dodoma
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, amekutana na kufanya mazungumzo na Ujumbe kutoka Benki ya Dunia kuhusu ushirikiano wa kimaendeleo kati ya Tanzania na Benki hiyo, kikao ambacho kilifanyika katika Ofisi za Wizara ya Fedha, Treasury Square, jijini Dodoma.
Katika kikao hicho wamejadiliana kuhusu kuendeleza mageuzi ya kimfumo yanayolenga uthabiti wa kiuchumi, uboreshaji wa fedha za umma, uhimilivu wa deni la serikali, kukuza sekta binafsi katika ujumuishaji wa kijamii katika masuala ya kiuchumi na uangalizi wa mabadiliko ya tabianchi.
Kikao hicho kilihudhuriwa na Kamishna wa Idara Usimamizi wa Deni la Serikali, Wizara ya Fedha, Bw. Japhet Justine, Kamishina wa Sera, Wizara ya Fedha, Dkt. Johnson Nyella, Kamishna Msaidizi wa Idara ya Usimamizi wa Deni la Serikali, Wizara ya Fedha, Bw. Nuru Ndile na viongozi wengine waandamizi wa Serikali na Benki ya Dunia.
No comments:
Post a Comment