
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa leo Juni 23, 2025 amemwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Utumishi wa Umma yanayofanyika katika viwanja vya Chinangali Park Jijini Dodoma
Katika hafla hiyo, Mheshimiwa Majaliwa atazindua mifumo miwili ambayo ni Mfumo wa kielektroni unaowezesha mifumo ya Serikali kuwasiliana na kubadilishana taarifa, ujulikanao kama Government Enterprises Service Bus (GovESB) na Mfumo wa pili ni wa e-Wekeza unaomuwezesha Mtumishi wa Umma kuwekeza katika Mfuko wa Faida (Faida Fund).
Siku ya Utumishi wa Umma husherehekewa kila Juni 23 kila mwaka na nchi wanachama wa Umoja wa Afrika kwa lengo la kutambua mchango wa Watumishi wa Umma katika maendeleo ya nchi zao na Bara la Afrika kwa ujumla.
Kaulimbiu ya maadhimisho hayo ni _“Himiza Matumizi ya Mifumo ya Kidijiti ili Kuongeza Upatikanaji wa Taarifa na Kuchagiza Uwajibikaji”




No comments:
Post a Comment