Na Mwandishi Wetu, Singida
Naibu Waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhe. Zainab Katimba (Mb) amesema kukamilika kwa utekelezaji wa miradi ya uboreshaji miundombinu ya Miji Tanzania (TACTIC) awamu ya pili kwenye Manispaa ya Singida kutaleta mabadiliko chanya kwenye huduma, manunuzi na mazingira bora ya kufanyia biashara kwa wajasiriamali na wafanyabiashara wa mkoa wa Singida.
Mhe. Katimba amebainisha hayo leo Juni 02, 2025, mkoani Singida mara baada ya kushuhudia utiaji saini mkataba wa ujenzi wa soko la Kimataifa la Vitunguu, ujenzi wa barabara za katikati ya Mji na Viwandani (Km 7.52), ujenzi wa mtaro wa maji ya mvua wa Km. 2.6 pamoja na Ofisi ya uratibu.
Akizungumzia Ujenzi wa soko la Vitunguu, Mhe. Katimba amebainisha kwamba jengo litakalojengwa litakuwa la ghorofa mbili, likiwa na maeneo maalum ya kuchambua na kukaushia vitunguu, maduka na vyumba vya huduma za kifedha, likiwa na uwezo wa kuhudumia wafanyabiashara 3000 kwa wakati mmoja, makadirio yakiwa ni kuingiza mapato ya Milioni 505 kwa mwaka tofauti na Milioni 300 za sasa zinazotokana na wafanyabiashara 1069 wanaoweza kuhudumiwa na soko la sasa.
Aidha, katika maelezo yake kando ya kupongeza waratibu wa mradi huo kwa kutoa nafasi kwa mkandarasi mzawa, Mhe. Katimba amemuagiza Mkandarasi M/s Sihotech Engeneering Company Limited kukamilisha mradi huo kwa wakati, ili tija ionekane mapema kwa wananchi wanaotarajiwa kuwa wanufaika wa mradi huo.
=
Pia amewasihi wananchi wa Manispaa ya Singida kutoa ushirikiano kwa Mkandarasi anayetekeleza mradi huo pamoja na kutunza miundombinu hiyo pale itakapokamilika ili iweze kuwa na tija iliyokusudiwa na kwa muda mrefu zaidi, akiziagiza Halmashauri zote zenye miradi ya TACTIC kusimamia vyema uendeshaji wa masoko na Vituo vya Mabasi ili kuzalisha mapato yaliyotarajiwa na Serikali kwa maendeleo ya maeneo yao.

No comments:
Post a Comment