Waziri Aweso akabidhiwa vikombe vya Mei Mosi 2025 - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, June 26, 2025

Waziri Aweso akabidhiwa vikombe vya Mei Mosi 2025


Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) amekabidhiwa vikombe vya ushindi vilivyopatikana katika mashindano ya Mei mosi 2025 yaliyofanyika mkoani Singida.  

Vikombe hivyo vimekabidhiwa na Mwenyekiti wa Timu ya Wizara ya Maji (Maji Sport) Jacob Kingazi katika ofisi za Wizara ya Maji Mtumba, Jijini Dodoma. 

Kingazi katika hafla hiyo amesema hamasa na uongozi makini wa Waziri Aweso umekua chachu ya mafanikio yaliyoletwa na wachezaji.  

“Mheshimiwa Waziri, licha ya kujenga misingi imara ambayo imewezesha mafanikio makubwa katika sekta ya maji, bado umekuwa chachu ya mafanikio katika eneo la michezo. Daima tutaendelea kujivunia uwepo wako ndani ya sekta na utaendelea kuwa mfano dhabiti kwa vizazi hata vizazi.” Kingazi amesema

Ameongeza Maji Sport bado inamipango mingi ya kuhakikisha michezo inaenda sambamba na mafanikio makubwa katika sekta ya maji na hivyo bado ushauri na hamasa zaidi zinahitajika kutoka kwa viongozi.

Waziri Aweso amesema michezo ni burudani, michezo ni afya na michezo ni umoja na faraja katika jamii, hivyo inapaswa kuendelezwa zaidi.

 Amesema michezo inaweza kuwa njia nzuri na sahihi zaidi katika kufikisha ujumbe kwa jamii hivyo viongozi wa Maji sport wahakikishe wanabuni mikakati imara ya kuhakikisha yote hayo yanafanikishwa.

Amesisitiza kuwa yeye ataendelea kutoa ushirikiano ili kuleta mafanikio yaliyoanzishwa katika michezo ndani ya sekta ya maji yanaendelezwa zaidi kama ambavyo tangu awali aliapa kuhakikisha sekta ya maji inapiga hatua kubwa.
 
Katika mashindano ya Mei Mosi 2025 yaliyofanyika mkoani Singida, Wizara ya Maji ilipata ushindi wa vikombe vitatu pamoja na medali tano.

No comments:

Post a Comment