WIZARA YA FEDHA KUKUSANYA JUMLA YA TRILIONI 50.17 - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, June 4, 2025

WIZARA YA FEDHA KUKUSANYA JUMLA YA TRILIONI 50.17


Wizara ya Fedha imekadiriwa kutafuta na kukusanya jumla ya shilingi trilioni 50.17, ikiwa ni mapendekezo ya bajeti ya wizara hiyo na Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi kwa mwaka 2025/2026.

Hayo yameelezwa leo Juni 04, 2025 na Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulu Nchemba bungeni Jijini Dodoma wakati akisoma hotuba ya bajeti ya Wizara ya Fedha kwa mwaka 2025/2026.

Dkt. Nchemba amesema kati ya fedha hizo, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) inatarajiwa kukusanya jumla ya shilingi trilioni 34.10, misaada shilingi trilioni 1.07, mikopo nafuu na ya kibiashara kutoka vyanzo vya ndani na nje shilingi trilioni 14.95 na maduhuli shilingi bilioni 53.54.

Aidha, Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi inakadiriwa kukusanya shilingi milioni 843, ikiwa ni ukodishaji wa kumbi za mikutano na kodi ya pango kutokana na upangishaji wa majengo ya ofisi yaliyopo katika mikoa mbalimbali nchini.

No comments:

Post a Comment