Mkurugenzi Mkazi, Amref Tanzania, Dkt. Florence Temu (wa pili kushoto) akiambatana na Dkt. Ndekya Oriyo kutoka Amref Tanzania wakati wa Ufunguzi wa Mkutano wa Mwaka wa Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete, jijini Dodoma.
Picha ya Pamoja ya wadau na Mgeni rasmi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Philip Isdor Mpango wakati wa Ufunguzi wa Mkutano wa Mwaka wa Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete, jijini Dodoma
Picha ya Pamoja ya wadau na Mgeni rasmi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Philip Isdor Mpango wakati wa Ufunguzi wa Mkutano wa Mwaka wa Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete, jijini Dodoma.
Picha ya Pamoja ya wadau na Mgeni rasmi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Philip Isdor Mpango wakati wa Ufunguzi wa Mkutano wa Mwaka wa Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete, jijini Dodoma.
***
Dodoma, Julai 12, 2025 Amref Health Africa nchini Tanzania imeshiriki katika ufunguzi wa mkutano wa mwaka wa Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri unaofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete, jijini Dodoma wenye kaulimbiu: “Wajibu wa Waganga Wakuu katika Kuimarisha Ubora wa Huduma za Afya kuelekea Bima ya Afya kwa Wote.”
Mgeni rasmi katika hafla hiyo alikuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Philip Isdor Mpango, ambaye aliwasili ukumbini leo Julai 12, 2025, na kupokelewa na viongozi mbalimbali wa serikali, wadau wa afya na wawakilishi kutoka mashirika ya maendeleo.
Akifungua mkutano huo, Mgeni rasmi Mheshimiwa Dkt. Philip Isdor Mpango amesisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya Serikali, wadau wa afya na jamii katika kuimarisha huduma za afya nchini.
Ameeleza kuwa Serikali itaendelea kuweka mazingira wezeshi kwa wataalamu wa afya ili kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi, huku akitambua mchango muhimu wa wadau wa afya katika kuleta ubunifu, kujenga uwezo na kufikia wananchi walioko pembezoni.
Amebainisha kuwa mkutano huo ni jukwaa muhimu la kushirikiana na kuweka mikakati ya pamoja kwa ajili ya kuhakikisha upatikanaji wa huduma bora za afya kwa wananchi wote.
Akizungumza katika mkutano huo, Mkurugenzi Mkazi wa Amref Tanzania, Dkt. Florence Temu, ameeleza kuwa ushiriki wa Amref Tanzania katika mkutano huu ni sehemu ya kuendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika kuimarisha mifumo ya afya ngazi ya jamii, mikoa na halmashauri.
“Mkutano huu ni jukwaa muhimu kwa ajili ya kufanya tathmini ya utekelezaji wa huduma za afya, kujadili changamoto na mafanikio, pamoja na kuweka mikakati ya pamoja ya kuimarisha utoaji wa huduma bora kwa wananchi,” amesema Dkt. Temu.
Mkutano wa Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri umeanza Julai 11, 2025, na unatarajiwa kuhitimishwa Julai 14, 2025.
Mkutano huu umewakutanisha wadau mbalimbali kutoka sekta ya afya wakiwemo viongozi wa serikali, mashirika ya kiraia, washirika wa maendeleo na wataalamu wa afya, kwa lengo la kuimarisha ushirikiano na kuweka mikakati shirikishi katika kuboresha huduma za afya nchini.
Amref Tanzania itaendelea kushirikiana kwa karibu na Serikali katika kuimarisha na kuboresha afya ya umma nchini. Kupitia ushirikiano wa kimkakati, ubunifu, na mbinu zinazozingatia jamii, Amref itaendelea kufanya kazi kuhakikisha upatikanaji wa huduma bora za afya kwa wote nchini Tanzania.
No comments:
Post a Comment