TANZANIA YAPOKEA MSAADA WA Sh. BILIONI 78.6 KUTOKA UJERUMANI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, July 9, 2025

TANZANIA YAPOKEA MSAADA WA Sh. BILIONI 78.6 KUTOKA UJERUMANI

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba (kulia), na Mkurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya Ujerumani (KfW) anaesimamia nchi za Afrika Mashariki na Umoja wa Ulaya, Bw. Christoph Tiskens, wakisaini Hati za Mikataba mitatu ya misaada yenye thamani ya euro milioni 25.68 (sawa na sh. bilioni 78.58) kwa ajili ya miradi ya maji, Mradi wa ustahimilivu wa tabianchi unaojulikana kama “Climate Resilient Towns project” na Uhifadhi wa Maliasili unaojulikana kama “Project for Sustainable Development of Protected Areas”, katika ukumbi wa Mikutano wa Ofisi Ndogo ya Wizara ya Fedha, jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba (kulia), Naibu Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Mhe. Manuel Muller (kushoto), na Mkurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya Ujerumani (KfW) anaesimamia nchi za Afrika Mashariki na Umoja wa Ulaya, Bw. Christoph Tiskens, wakionesha Hati za Mikataba mitatu ya misaada yenye thamani ya euro milioni 25.68 (sawa na sh. bilioni 78.58) kwa ajili ya miradi ya maji, Mradi wa ustahimilivu wa tabianchi unaojulikana kama “Climate Resilient Towns project” na Uhifadhi wa Maliasili unaojulikana kama “Project for Sustainable Development of Protected Areas”, baada ya kusaini hati hizo katika ukumbi wa Mikutano wa Ofisi Ndogo ya Wizara ya Fedha, jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, akizungumza baada ya kusaini kwa niaba ya Serikali, Hati za Mikataba mitatu ya misaada yenye thamani ya euro milioni 25.68 (sawa na sh. bilioni 78.58) kwa ajili ya miradi ya maji, mradi wa ustahimilivu wa tabianchi unaojulikana kama “Climate Resilient Towns project” na Uhifadhi wa Maliasili unaojulikana kama “Project for Sustainable Development of Protected Areas”, iliyotolewa na Benki ya Maendeleo ya Ujerumani KfW, jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya Ujerumani (KfW) anaesimamia nchi za Afrika Mashariki na Umoja wa Ulaya, Bw. Christoph Tiskens, akizungumza jambo baada ya kusaini Hati za Mikataba mitatu ya misaada yenye thamani ya euro milioni 25.68 (sawa na sh. bilioni 78.58) kwa ajili ya miradi ya maji, mradi wa ustahimilivu wa tabianchi unaojulikana kama “Climate Resilient Towns project” na Uhifadhi wa Maliasili unaojulikana kama “Project for Sustainable Development of Protected Areas”, iliyotolewa na Benki hiyo, katika ukumbi wa wa Mikutano wa Ofisi Ndogo ya Wizara ya Fedha, jijini Dar es Salaam.

Naibu Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Mhe. Manuel Muller, akizungumza jambo wakati wa hafla ya utiaji Saini wa Mikataba mitatu ya misaada yenye thamani ya euro milioni 25.68 (sawa na sh. bilioni 78.58) katika ya Serikali ya Tanzania na Ujerumani, kupitia Benki yake ya Maendeleo ya KfW, kwa ajili ya miradi ya maji, mradi wa ustahimilivu wa tabianchi unaojulikana kama “Climate Resilient Towns project” na Uhifadhi wa Maliasili unaojulikana kama “Project for Sustainable Development of Protected Areas”, katika ukumbi wa Mikutano wa Hazina Ndogo, jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba (Katikati mstari wa mbele), Katibu Mkuu Wizara ya Maji (wa pili kushoto mstari wa mbele), Naibu Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Mhe. Manuel Muller (wa pili kulia mstari wa mbele), na Mkurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya Ujerumani (KfW) anayesimamia nchi za Afrika Mashariki na Umoja wa Ulaya, Bw. Christoph Tiskens (wa kwanza kushoto mstari wa mbele), wakiwa katika picha ya pamoja na Maafisa waandamizi wa Serikali ya Tanzania na Serikali ya Ujerumani, baada ya hafla ya utiaji saini Mikataba mitatu ya misaada yenye thamani ya euro milioni 25.68 (sawa na sh. bilioni 78.58) kwa ajili ya miradi ya maji, mradi wa ustahimilivu wa tabianchi unaojulikana kama “Climate Resilient Towns project” na Uhifadhi wa Maliasili unaojulikana kama “Project for Sustainable Development of Protected Areas”, baada ya kusaini hati hizo katika ukumbi wa Hazina Ndogo, jijini Dar es Salaam.


(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Dar es Salaam)


Na. Peter Haule na Joseph Mahumi, WF, Dar es Salaam


Tanzania na Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani kupitia Benki ya Maendeleo ya Ujerumani (KFW) zimesaini Mikataba mitatu ya misaada yenye thamani ya Euro milioni 25.68 (sawa na sh. Bilioni 78.58) kwa ajili ya miradi ya Maji na Maliasili.

Mikataba hiyo imesainiwa katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba na kwa upande wa Ujerumani imesainiwa na Naibu Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Mhe. Manuel Muller na Mkurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya Ujerumani (KfW) anaesimamia nchi za Afrika Mashariki na Umoja wa Ulaya, Bw. Christoph Tiskens.

Dkt. Mwamba alisema kuwa mikataba iliyosainiwa ni kwa ajili ya mradi wa programu ya ufadhili wa miradi ya Maji inanayotegemea matokeo (Investment Financing Facility – Output Based Approach (IFF-OBA) kwa kiasi cha Euro milini 10 sawa na shilingi za Tanzania bilioni 30.6.

Mkataba mwingine ni wa fedha za kufanya upembuzi yakinifu kwa ajili ya mradi wa ustahimilivu wa tabia nchi (Climate Resilient Towns project) kwa kiasi cha shilingi za Tanzania bilioni 2.08.

Alisema kuwa mkataba wa tatu ni wa utekelezaji wa mradi wa Uhifadhi wa Maliasili unaojulikana kama Project for Sustainable Development of Protected Areas kwa kiasi cha Euro milioni 15 sawa na shilingi bilioni 45.9.

Amesema lengo la miradi hiyo ni kutoa motisha kwa Mamlaka za Maji hapa Tanzania kukopa kutoka Benki za Kibiashara kwa ajili ya kujenga miundombinu ya maji ili kuboresha huduma na kuongeza mapato.

Alisema kuwa Kupitia Programu ya IFF – OBA, mamlaka zilizokidhi vigezo zinaweza kukopa kutoka Benki za Biashara na kupatiwa ruzuku kutoka kwenye programu ambapo Mamlaka husika zinapokidhi vigezo, zinaweza kupatiwa ruzuku ya asilimia 50 ya gharama za miradi hadi kufikia kiwango kisichozidi Euro milioni Moja.

Pia mikataba hiyo inalenga uhifadhi na uendelezaji wa maeneo ya Hifadhi za Serengeti na Katavi- Mahale kuhakikisha kunakuwa na uhifadhi na manufaa ya kijamii kwa jamii zinazozunguka hifadhi hizo.

Aidha Dkt. Mwamba ameihakikishia Serikali ya Ujerumani kuwa miradi iliyokusudiwa itatekelezwa kikamilifu na pia Tanzania chini ya Uongozi wa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kuendelea kuimarisha ushirikiano wa kimaendeleo na Ujerumani kwa manufaa ya watu wa pande zote mbili.

Kwa Upande wake Naibu Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Mhe. Manuel Muller, alisema kuwa utiaji saini wa mikataba hiyo mitatu ambayo ni sehemu ya muendelezo wa ushirikiano wa kifedha kati ya Tanzania na Ujerumani kupitia benki yake ya maendeleo (KfW).

“Nina furaha kubwa kufanikisha zoezi hili na Ninawatakia wananchi wa Tanzania maendeleo makubwa, hasa katika Maliasili ambayo pia inamaanisha utalii kuna watalii wengi kutoka Ulaya, hasa kutoka Ujerumani, na hiyo inaleta nguvu kubwa ya kiuchumi kwa nchi, jambo ambalo ni muhimu. Naweza kuwahakikishia kuwa Ujerumani itaendelea kuwa mshirika wa kweli wa Tanzania, Tutaendelea kusimama pamoja nanyi” alisema Mhe. Muller

Naye Mkurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya Ujerumani (KfW) anaesimamia nchi za Afrika Mashariki na Umoja wa Ulaya, Bw. Christoph Tiskens, alisema kuwa Mikataba hiyo, ni ishara ya hatua nyingine mbele katika ushirikiano kati ya Tanzania na Ujerumani ambao umekuwa mzuri tangu miaka ya 1960.

Bw. Christoph Tiskens alisema kuwa, mikataba hiyo miwili itagusa sekta muhimu sana kwa maendeleo ya Tanzania, kupitia awamu ya pili ya Mfuko wa Uwekezaji wa Fedha kwa ajili ya Miundombinu ya Maji (Investment Financing Facility) yenye thamani ya Euro milioni 10, ambayo itafungua fursa mpya kwa mamlaka za maji hapa Tanzania kupitia benki za ndani.

“Kipengele cha kupitia benki za ndani ni muhimu sana kwa sababu mbinu hii ya ubunifu inasaidia kukuza miradi inayoweza kufadhiliwa (bankable projects) kwa ajili ya mamlaka za maji, hasa katika mazingira ambayo Tanzania inahitaji kiasi kikubwa cha uwekezaji na fedha” alisema Bw. Tiskens.

Aliongeza kuwa Mkataba wa pili uliouwekwa saini, unaoitwa "Maendeleo Endelevu ya Mfumo wa Ikolojia ya Maeneo ya Hifadhi", utaimarisha ushirikiano wa nchi hizo mbili pamoja na wadau wa hapa nchini, na mkataba huo unalenga kuimarisha uhifadhi wa maliasili amba oni urithi wa kipekee wa Tanzania na pia kuanzisha minyororo ya thamani kwa ajili ya wananchi wanaoishi karibu na maeneo haya ya asili ya maliasili, ili kuchochea ukuaji wa uchumi na kuleta ajira.

No comments:

Post a Comment