Na. Jeremiah Mbwambo, GITEGA-BURUNDI
Waziri wa Afya Burundi Dr. Baradahana Lydwine amefungua kambi maalumu ya madaktari Bingwa wa Hospitali ya Benjamin Mkapa inayo fanyika Burundi katika Mkoa wa Gitega na baadae Burundi
"Nimefarijika sana kuwaona madaktari Bingwa wa Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH) wakitoa matibabu kwa wananchi wa Burundi, nikupongeze Mheshimiwa Balozi wa Tanzania nchini Burundi na Uongozi wa BMH kwa kuratibu zoezi hili mpaka kufanikiwa" alisema Mhe. Lydwine
Ameongeza kuwa CRDB wamekuwa na mchango mkubwa kuwezesha kambi hii kufanyika
"Siwezi acha kuwataja CRDB kwa namna walivyo wezesha kifedha kufanikisha kambi hii tunawashukuru kwa moyo wa kujali" alisema Mhe. Lydwine
Kwa upande wake Balozi wa Tanzania nchini Burundi Mhe. Gelasius Byakanwa amewasilisha salamu za Mhe. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
"ninapowasilisha salamu hizi kutoka kwa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kunausemi unasema kizuri kula na nduguyo Mhe. Rais amefanya uwekezaji mkubwa katika vifaa tiba vya kisasa na amesomesha madaktari, ameona sasa kunaumuhimu wa kuleta hizi huduma katika nchi jirani zinazo izunguka Tanzani, pia ameniambia sasa siyo lazima msafiri kwenda mbali kufuata matibabu wakati huduma zote za ubingwa zinatolewa Hospitali ya Benjamin Mkapa, ni wewe kuamua kwenda na uzuri wake ukitoka asubuhi Burundi jioni unakuwa umeshafika" alisema Balozi Byakanwa
Aidha Mkurugenzi Mtendaji Prof. Abel Makubi ameelezea utayari wa Hospitali ya Benjamin Mkapa kufanya kambi maalumu katika nchi zinazoizunguka Tanzania na kujengea uwezo na kutaaluma kwa watumishi wa nchi hizo.
"Tunamshukuru Mhe. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutuwezesha Hospitali ya Benjamin Mkapa kwa kutupatia vifaa tiba na kusomesha wataalamu wetu kwa uwezo tulionao sasa tunaweza kusogeza huduma kwenye nchi zinazo tuzunguka, tupo tayari na hata tukialikwa tutakuja maana huduma zote tunaweza kuzileta kwenye uhitaji" alisema Prof. Makubi.
No comments:
Post a Comment