Tutaendelea na sera yetu ya elimu bila ada ili watoto wetu waweze kusoma vizuri. Tutatoa shilingi Bilioni mbili na Milioni mia sita kama mikopo kwa wanawake, vijana na wenye ulemavu wapatao 8, 320 ili kuwaongezea mitaji kwaajili ya kujinyanyua kiuchumi. Tutaanzisha viituo viwili vya kukodisha zana za kilimo ili kupunguza gharama za uzalishaji na kuwezesha upatikanaji wa matrekta 50 kwaajili ya wakulima na tunaweka vituo hivi kwasababu wenye matrekta yao huko ukienda kulikodi ni Milioni 30 kwa hekta, serikali tunaweka vituo hivi tunakwenda nusu ya bei ya mkodishaji binafsi kwahiyo itawarahisishia wakulima kupatikana kwa trekta na zana za kilimo lakini pembejeo za kilimo zitakuwepo kwenye vituo hivyo
Tutaendelea pia kusogeza umeme karibu zaidi na wananchi kwa kuunganisha vitongozi vyote 735."- Rais Samia Suluhu Hassan na Mgombea Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM akiwa Ngerengere Mkoani Morogoro kwenye Kampeni leo Ijumaa Agosti 29, 2025.
No comments:
Post a Comment