Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mgombea Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, Dkt. Samia Suluhu Hassan ameahidi kutoa kipaumbele cha upatikanaji wa maji safi na ya uhakika kwa wakazi wa Morogoro, akihimiza ushirikiano wa pamoja katika kutunza mazingira.
Rais Samia ameeleza hayo leo Ijumaa Agosti 29, 2025 wakati akiwa kwenye Kampeni za Chama Cha Mapinduzi Mkoani Morogoro, akibainisha kufahamu changamoto iliyopo kwenye maeneo ya Dutumi, Mvua na Kisaki na kubainisha kuwa maeneo hayo ni muhimu kwa Kilimo cha Umwagiliaji na sasa limeathirika kutokana na ukataji mkubwa wa miti unaotokana na mahitaji ya mkaa na kuni kwaajili ya kupikia.
Aidha akirejea ombi la aliyekuwa Mbunge wa Morogoro Kusini Mashariki Mhe. Hamisi Shaban Taletale, Rais Samia amesisitiza kuwa mara baada ya wananchi kumpa ridhaa ya kuongoza tena serikali atasimamia kikamilifu ujenzi wa barabara ya Bigwa, Mvua Kisaki ili ijengwe na kukamilika kwa wakati, kama sehemu ya kuchochea shughuli za kiuchumi na Kijamii kwenye eneo hilo la Mkoa wa Morogoro.
No comments:
Post a Comment