TARURA YAENDELEA KULETA FURSA KWA WANANCHI KUPITIA MRADI WA RISE - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Friday, August 22, 2025

TARURA YAENDELEA KULETA FURSA KWA WANANCHI KUPITIA MRADI WA RISE



Na Mwandishi Wetu, Pangani, Tanga


Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) kupitia mradi wa Uboreshaji Barabara za Vijijini kwa Ushirikishaji wa Jamii na Ufunguaji wa Fursa za Kijamii na Kiuchumi (RISE) umeendelea kuleta fursa kwa kuwapatia mafunzo vikundi 14 vya wakazi wa kata ya Pangani ya zamani, wilayani Pangani mkoani Tanga.

Mafunzo hayo yanalenga kuwapatia vikundi hivyo fursa na elimu ya umuhimu wa wananchi kushiriki moja kwa moja kwenye matengenezo na maboresho ya kazi mbalimbali kupitia programu ya CBRM (Community Based Road Maintenance)

Kupitia programu hiyo wananchi walio wanachama wa vikundi hivyo watapata fursa ya kukua kichumi na kijamii kupitia mafunzo mbalimbali na ajira kwa vikundi hivyo.

Akizungumza wakati wa mafunzo hayo, Meneja wa TARURA wilaya ya Pangani, Mhandisi Mwita Muhochi ameeleza umuhimu wa ushirikishwaji wa wananchi katika matengenezo na utunzaji wa miundombinu ya barabara.

Aidha, Mhandisi Delchance Nuru kutoka Timu ya mradi wa RISE, ameeleza kuhusu mradi wa RISE na kufafanua zaidi kuhusu programu kwa vikundi hivyo.

Mafunzo hayo yanafanyika kwa kuhusisha mafunzo ya darasani pamoja na kujifunza kwa vitendo.



No comments:

Post a Comment