
Na Mwandishi Wetu, Handeni
MKUU wa Wilaya ya Handeni, Mhe. Salum Nyamwese, amekagua ujenzi wa Chuo cha Ufundi Stadi (VETA) wilayani humo na kuagiza maboresho mbalimbali kwenye utekelezaji wa mradi huo unaotarajiwa kugharimu Sh.Bilioni 1.6.
Miongoni mwa maboresho ni kuangalia namna ya kuhakikisha bweni linajumuishwa katika awamu ya kwanza ya ujenzi, ili wanafunzi waweze kuanza kupata mafunzo mara tu awamu hiyo itakapokamilika.
Akizungumza baada ya kukagua mradi huo, Nyamwese amewataka mshauri elekezi na msimamizi wa mradi kushirikiana kuhakikisha bweni linaingizwa katika mpango huo kutoka na awamu ya kwanza inayohusisha majengo tisa kutokuwa na bweni.
Vilevile, ameelekeza Jeshi la Zimamoto lishirikishwe mapema kutoa ushauri kuhusu vifaa vya usalama vinavyohitajika kabla ya mradi kukamilika.
Hata hivyo, amewapongeza wasimamizi wa mradi kwa kazi nzuri iliyofanyika, akisisitiza mapungufu yaliyojitokeza yashughulikiwe mara moja.







No comments:
Post a Comment