KISHINDO CHA KAMPENI ZA DKT. SAMIA KUTIMUA VUMBI MTWARA MJINI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Friday, September 26, 2025

KISHINDO CHA KAMPENI ZA DKT. SAMIA KUTIMUA VUMBI MTWARA MJINI


Mgombea wa nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo Ijumaa Septemba 26, 2025 anatarajiwa kuwa na Mkutano mkubwa wa Kampeni Mtwara Mjini, Mkoani Mtwara, akitarajiwa kueleza mafanikio ya serikali ya awamu ya sita pamoja na yale ambayo Chama Cha Mapinduzi wamepanga kuyafanya ikiwa watepewa ridhaa kupitia uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025.

Jana Alhamisi akiwa Lindi Mjini kwenye Viwanja vya Ilulu, Dkt. Samia pamoja na kuahidi kuendelea kutoa huduma muhimu za kijamii kwa wananchi, amewahakikishia pia Watanzania kuwa mradi mkubwa wa kuchakata na kusindika gesi asilia kuwa kimiminika (LNG) umekaribia kuanza utekelezaji wake, akisema mradi huo ni mkubwa ukiwa na thamani ya Dola za Marekani Bilioni 40 sawa na Shilingi trilioni 100 na hivyo serikali ilitaka kuwa na uhakika wa manufaa kabla ya kuanza utekelezaji wake.

Kuhusu Uvuvi Mkoa wa Lindi, Dkt. Samia amebainisha kuwa ujenzi wa bandari ya Uvuvi Kilwa unaoendelea, utakapokamilika utatoa ajira 30,000 na kufungua fursa za Viwanda vya kuchakata samaki lakini pia serikali ina mpango wa kujenga kiwanda cha kusindika samaki kando ya ujenzi wa Kongani za Viwanda kila Wilaya ambazo zitakuwa zinaongeza thamani ya mazao ya kilimo, misitu na uvuvi.

Kwa Mtwara Mjini CCM na Dkt. Samia wameahidi Kujenga meli ya mizigo kutoka Mtwara hadi Visiwa vya Comoro, Ujenzi wa reli ya kisasa ya SGR kutoka bandari ya Mtwara hadi Mbambabay na Songea hadi Ludewa ili kuunganishwa na mradi wa makaa ya mawe, upanuzi wa uwanja wa ndege Mtwara kwa awamu ya pili ikijumuisha ujenzi wa jengo la abiria la kisasa, mnara wa kuongozea ndege, jengo la kituo cha zimamoto na jengo la kituo cha hali ya hewa, ukamilishaji wa jengo la utawala Halmashauri ya Mtwara.

Wameahidi pia Ujenzi wa maghala 7 ya kuhifadhia mazao, Ujenzi wa jengo la maonesho ya kilimo la Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara, Ujenzi wa skimu ya umwagiliaji Arusha chini, Uboreshaji wa miundombinu ya Maji Mji wa Mtwara, ujenzi wa kiwanda cha sukari katika bonde la Mto Kitere, ujenzi wa kiwanda cha kubangua korosho, mradi mkubwa wa kutoa maji mto Ruvuma hadi Mtwara.

Aidha Ilani ya Chama Cha Mapinduzi CCM imeahidi pia Upimaji na Upangaji Mji, Ujenzi daraja la Kilambo (Tanzania- Msumbiji border), ujenzi barabara ya Mangamba- Madimba (Km 35.63) na Madimba- Tangazo (Km16.87), Ujenzi wa Machinjio 3 ya kisasa, uendelezaji wa Hospitali ya Kanda Mtwara, ukamilishaji wa majengo ya Hospitali ya Manispaa ya Mtwara, Ujenzi wa vituo vya afya Kata ya Mtawanya, Mkutimango na Ndumbwe, Namtumbuka, Mnima na Chawi na ujenzi wa Zahanati 12 Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara.

No comments:

Post a Comment