DKT. MPANGO AONGOZA UJUMBE WA TANZANIA MKUTANO WA TABIANCHI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Sunday, September 7, 2025

DKT. MPANGO AONGOZA UJUMBE WA TANZANIA MKUTANO WA TABIANCHI



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango, leo tarehe 07 Septemba 2025 amewasili Jijini Addis Ababa nchini Ethiopia, kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa Pili wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Nchi za Afrika kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi.

Mkutano huo utakaoanza tarehe 08 hadi 10 Septemba 2025, pamoja na mambo mengine, unalenga kuimarisha sauti ya Afrika katika mijadala na majukwaa ya kimataifa; kuimarisha uhimilivu na ustamilivu dhidi ya mabadiliko ya tabinchi barani Afrika; na, kuimarisha juhudi na ubunifu barani Afrika katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Mkutano huo utahudhuriwa na Wawakilishi wa Serikali za Nchi wanachama wa Umoja wa Afrika na nchi nyingine duniani; Wawakilishi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa; Wadau wa Maendeleo; Mashirika yasiyo ya Kiserikali; Sekta Binafsi; Asasi za Kiraia; Taasisi za elimu ya juu na utafiti pamoja na Wawakilishi wa Jamii asilia.

Vilevile, Makamu wa Rais anatarajiwa kushiriki katika Mikutano ya Uwili yenye lengo la kuimarisha ushirikiano baina ya Tanzania, Mataifa na Mashirika mbalimbali yanayoshiriki Mkutano huo.





No comments:

Post a Comment