
MGOMBEA Mwenza wa Kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, amewasili wilayani Ludewa mkoani Njombe,leo Jumatatu Septemba 22,2025 kuendelea na mikutano yake ya kampeni akitokea Mkoa wa Ruvuma.
Dkt.Nchimbi amewasili kwenye uwanja wa mpira wa Ludewa na kupokewa na Viongozi waandamizi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kuwasalimia Wananchi kabla ya kuwahutubia.
Akiwa katika mkutano huo,Dkt Nchimbi ambae ni Mgombea Mwenza wa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan pamoja na mambo mengine atawahutubia Wananchi wa jimbo la Ludewa na kuwanadi Wagombea Ubunge wa majimbo ya Mkoa huo,akiwemo mgombea Ubunge wa jimbo la Ludewa,Ndugu Joseph Zacharius Kamonga na Madiwani.
Dkt. Nchimbi anaendelea kuinadi Sera na Ilani ya CCM ya Uchaguzi Mkuu 2025-2030,ambayo inakwenda kuboresha maisha ya wananchi na ustawi wa Maendeleo katika miaka mitano ijayo.
Aidha,amekuwa akitumia nafasi hiyo pia kuwaomba wananchi kumchagua mgombea Urais wa CCM,Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan, Wabunge na Madiwani wa Chama hicho kwa kura za kishindo ifikapo Oktoba 29,2025






No comments:
Post a Comment