KATIBU MKUU WA MADINI ATEMBELEA BANDA LA GST KWENYE MAONESHO YA MADINI GEITA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Monday, September 22, 2025

KATIBU MKUU WA MADINI ATEMBELEA BANDA LA GST KWENYE MAONESHO YA MADINI GEITA



Na Mwandishi Wetu, Geita


Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Mhandisi Yahya Samamba, ametembelea Banda la GST katika Maonesho ya Nane ya Kitaifa ya Teknolojia ya Madini yanayoendelea kwenye Viwanja vya Dkt. Samia Suluhu Hassan, Bombambili, Manispaa ya Geita.

Katika ziara hiyo, Mhandisi Samamba ameambatana na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Msafiri Mbibo.

Aidha Viongozi wengine waliotembelea banda la GST ni pamoja na Dkt. Mussa Budeba Mtendaji Mkuu wa GST, Mwenyekiti wa Tume ya Madini Dkt. Janet Lekashingo, pamoja na Makamishna wa Tume ya Madini Mhandisi Theonestina Mwasha na Dkt. Theresia Numbi.

Kupitia maonesho hayo GST Imeendelea kutoa elimu kwa wadau mbalimbali wa sekta ya Madini kuhusu teknolojia na mashine mbalimbali zinazotumika kwenye utafutaji na uchenjuaji wa madini.



No comments:

Post a Comment