KISHINDO CHA DKT. SAMIA KUTUA MKOANI SINGIDA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Tuesday, September 9, 2025

KISHINDO CHA DKT. SAMIA KUTUA MKOANI SINGIDA


Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Samia Suluhu Hassan leo Jumanne Septemba 09, 2025 anatarajia kuanza kunadi sera zake kwa wananchi wa Mkoa wa Singida katika maeneo ya Manyoni, Ikungi na kumalizia Singida Mjini.

Wakati huu kampeni ya CCM inakuja baada ya Mgombea huyo kukamilisha kampeni katika mikoa ya nyanda za juu kusini, mikoa ya Songwe, Mbeya, Njombe na Iringa ambao alibainisha sera zake kwa maelfu ya wananchi waliokuwa wakifurika kwenye mikutano yake akitumia mbinu ya kubainisha mafanikio ya serikali yake na ahadi kwa miaka mitano ijapo pindi wananchi watakapompa ridhaa ya kuunda serikali.

Katibu wa CCM, Mkoa wa Singida, Lucy Boniface amewaambia wanahabari kuwa maandalizi kwaajili ya mikutano hiyo yako vizuri na watampokea katika Wilaya ya Manyoni na kuelekea Ikungi na kisha atamalizia mkutano mkubwa katika uwanja wa Bombadia Singida Mjini

“Tumejipanga kumpokea kwa bashasha kubwa kwa vikundi vya hamasa wasanii na watu wengi wapo tayari kuhakikisha Mkoa wa Singida tunaweka historia,” alisema Katibu huyo wa CCM Mkoa.


Amesema siku inayofuata ataelekea Wilaya ya Iramba ambako atafanya mkutano mkubwa katika eneo la Misingiri na kisha kuelekea mkoani Tabora.

No comments:

Post a Comment