MD - DUWASA AWATAKA MAJI SPORTS CLUB KUWA NA MFUKO WA USHINDI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Tuesday, September 23, 2025

MD - DUWASA AWATAKA MAJI SPORTS CLUB KUWA NA MFUKO WA USHINDI


Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA) Mhandisi Aron Joseph, amewataka Maji Sports Club kuwa na Mfuko wake kwa lengo la kujihakikishia ushindi na kuendelea kuiheshimisha sekta ya maji katika michezo.

Mhandisi Aron ameyasema hayo baada ya wawakilishi wa Maji Sports Club kufika ofisini kwake wakiwa na makombe ya ushindi waliyoyapata katika mashindano ya SHIMIWI 2025 yaliyofanyika Jijini Mwanza ikiwa ni sehemu ya shukrani kwa ushirikiano aliyoutoa kwa wanamichezo hao, ambao walifanikiwa kutwaa ubingwa wa michezo ya RELAY (Nafasi ya Tatu kwa Upande wa Wanawake), Mchezo wa DARTS (Nafasi ya Kwanza kwa upande wa Wanaume), Mchezo wa BAO (Nafasi ya Pili kwa upande wa Wanawake) na Mchezo wa KARATA (Nafasi ya Kwanza kwa upande wa Wanawake).

Mhandisi Aron anasema "lazima tuwe na vyanzo vya fedha kwa ajili ya timu ya sekta ya maji ambavyo ni reliable na sio vya kuokoteza" lengo ni kutoa fursa kwa wanamichezo wote ambao wapo katika sekta ya maji, ila wanakwama kwa sababu ya kukosa rasilimali fedha.

Kwa upande wake Katibu wa Maji Sports Club Bw. James Kalimanzila amemshukuru Mkurugenzi Mtendaji wa DUWASA kwa kuiwezesha timu hiyo na kumuahidi kuwa watafanyia kazi suala la kunzishwa kwa Mfuko wa Maji Sports Club ili kuipa nguvu timu hiyo.


No comments:

Post a Comment