
Naibu Wakili Mkuu wa Serikali, Bi. Alice Mtulo akikata utepe kwa ajili ya kukabidhi gari kwa Wakili wa Serikali Mfawidhi wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali, Mkoa wa Manyara ndugu Lameck Butuntu katika makabidhiano yaliyofanyika Jijini Dodoma. Anayeshuhudia kushoto ni Wakili wa Serikali Mfawidhi Mkoa wa Manyara Ndugu. Lameck Butuntu.

Naibu Wakili Mkuu wa Serikali, Bi. Alice Mtulo akikabidhi funguo ya gari kwa Wakili wa Serikali Mfawidhi wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali, Mkoa wa Manyara ndugu Lameck Butuntu katika makabidhiano yaliyofanyika Jijini Dodoma.

Naibu Wakili Mkuu wa Serikali, Bi. Alice Mtulo (wa tatu kutoka kushoto) akiwa pamoja na Watumishi wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali Mkoa wa Manyara mara baada ya kukabidhi gari hiyo Jijini Dodoma. Wa Pili kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Madai ndugu Mark Mulwambo na kwanza kushoto ni Afisa Rasilimali Watu wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali Bi. Neema Baltazary.

Naibu Wakili Mkuu wa Serikali, Bi. Alice Mtulo akipeana mkono na Wakili wa Serikali Mfawidhi Mkoa wa Manyara mara baada ya kukabidhi gari hiyo Jijini Dodoma.
Na Mwandishi Wetu
Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali Manyara Yakabidhiwa Gari
Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali Mkoa wa Manyara imefanikiwa kupata gari mpya ambayo itasaidia kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yake ya kila siku kwa wakati.
Akizungumza mara baada ya kukabidhi gari hiyo aina ya Toyota Hilux Jijini Dodoma, Naibu Wakili Mkuu wa Serikali Bi. Alice Mtulo amesema kuwa uwepo wa gari hiyo utasaidia utekelezaji wa majukumu ya kila siku hatua itakayosaidia kuongeza tija, ufanisi na kuleta matokeo chanya yatakayosaidia Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali mkoani Manyara kufikia malengo iliyojiwekea kwa wakati.
Aliongeza kuwa uwepo wa gari hiyo ni jitihada za Serikali kupitia Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali kuboresha mazingira ya utendaji kazi hasa ukizingatia jiografia ya Mkoa huo ambapo Mawakili wamekuwa wakitumia muda mrefu kutoa huduma kutokana na umbali uliopo kutoka wilaya moja kwenda wilaya nyingine.
Kwa upande wake Wakili Mfawidhi wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali Mkoa wa Manyara ndugu Lameck Butuntu ameishukuru Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali kwa kuwapatia gari hiyo huku akifafanua kuwa gari hiyo itasaidia kupunguza changamoto za kiutendaji zilizokuwepo kwa kuwa sasa wataweza kutekeleza majukumu yao kwa wakati ikiwa ni pamoja na kutembelea maeneo mbalimbali ndani ya mkoa huo ikiwemo yale maeneo yaliyokuwa hayafikiki kwa wakati.
Alieleza kuwa, ujio wa gari hiyo utasaidia kutembelea wilaya, tarafa, Kata za mkoa huo kwa wakati ili kuhakikisha wanaisaidia Serikali na wananchi kupata haki kwa kutembelea maeneo yenye migogoro hatua itakayosaidia kuendesha na kumaliza mashauri hayo kwa wakati.
Aidha, Ndugu Butuntu alisema kuwa Mawakili wa Serikali mkoani humo sasa watafika mahakamani kwa wakati tofauti na awali ambapo iliwalazimu kuazima magari kutoka taasisi nyingine za Serikali.
Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali mkoani Manyara, inahudumia jumla ya Wilaya tano za Mkoa huo ambazo ni Wilaya ya Babati, Mbulu, Hanang’i, Kiteto na Simanjiro.
No comments:
Post a Comment